Shilole afunguka kupigana kwake

Shilole afunguka kupigana kwake

08 July 2019 Monday 12:12
Shilole afunguka kupigana kwake

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
MSANII, Zena Yusuf Mohammed, maarufu (Shilole) ameeleza  sababu ya  kupigana kwake katika hafla ya  kusheherekea kuzaliwa kwa mama Diamond na Tanasha, kuwa ni kuzarauliwa.

Jana Julai 7, 2019 katika viwanja vya Mlimani City jijini Dar es Salaam, msanii Nassib Abdul(Diamond) alianzimisha siku ya kuzaliwa mama yake mzazi na mpenzi wake Tanasha kwa kufanya sherehe maalum na kuwatunza kila mmoja gari aina ya V8 new modern zenye  thamani ya zaidi  milioni 300.

Wakati akiingia ukumbi hapo, akiwa katika njia ya kuingia gafla  Shilole alionekana akianza kupigana na mmoja wa walinzi waliokuwepo eneo hilo kabla ya kudhibitiwa na aliingia  ukumbini huku akiwa analalamika

Leo Julai 8, 2019, Shilole ameandika; "707 was super amazing Nilikuwa na wakati mzuri sana asante sana kaka angu Diamon platnumz kwa kunipa heshima kama wengine wengi waliojumuika pamoja na familia yako."

"Tukirudi kwenye suala la vile vichwa maana napokea simu nyingi za kutaka kujua kilichotokea jaman naomba niwajibu tu kwa ufupi kwanza niombe Radhi sana kwa WaTanzania na kila ambae suala hili lilimletea usumbufu maana vichwa ni vya kia shwazinega vile."

"By the way tulighafirika kwasababu ya namna tulivyopokelewa aisee tukawa kama vibaka tuliovamia shughuli alafu na kuanza kutaka kumdhalilisha mume wangu mpaka kumchania koti for what? Yani nikajikuta tu ule udada mwajuma ukaibuka nikalianzisha vagi."

"Tunashukuru Mungu yaliisha salama tuliyajenga tukaombana radhi. lakini hii kitu si nzuri, jamani hakuna wasanii wanaotokea shughuli ya msanii mwenzao bila kualikwa sisi ni familia unapoenda kwenye jambo la mwenzio ni kushow love na support hakuna anaekuja kwenye event zangu ukasikia anapata hiyo kero mlangoni kwasabu hakuna kitu kizuri kama uandae kitu chako alafu uone watu wako wamekuja kukusupport."

"Haya natumai mmeshapata maelezo nipumzisheni na maswal msije mkala vichwa na nyie.'

Updated: 08.07.2019 12:33
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.