Wasanii UDSM waaswa

Wasanii UDSM waaswa

16 June 2019 Sunday 08:58
Wasanii UDSM waaswa

Na Francis Peter, Dar es Salaam

WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm) wanaochukua Shahada ya Sanaa Bunifu wametakiwa kutumia vionjo vya asili vya nchini ili kujitofautisha na wa nje.

Pia wameaswa kulitumia Tamasha la Sanaa Blast kama fursa ya ajira kujiajiri baada ya kuhitimu masomo yao.

Hayo yamesemwa na Principal wa Ndaki ya Hisia- Idara ya Sanaa Bunifu wa chuo hicho, Dkt. Rose Upor katika Siku ya Kwanza ya tamasha hilo.

Amesema wanafunzi wanatakiwa kulitumia tamasha kama fursa  ya kuonyesha vipaji vyao kwenye sanaa ya muziki, uchoraji na uigizaji na kubainisha kabla au baada kuhitimu wana uwezo wa kujiajiri kutokana mafunzo ya vitendo waliyopata.

“Wanafunzi wanatakiwa kulitumia tamasha hili kujiajiri kwa sababu mafunzo wanayopata kwa vitendo kwenye taaluma yao yatawasaidia kujiajiri na kutengeneza ajira,” amesema Dkt. Rose.

Amesema lengo la tamasha hilo kuviendeleza vipaji vya wanafunzi wa taaluma hiyo, kuwawezesha wanafunzi kufanya sanaa ya vitendo baada ya kuhitimu pamoja kuwajengea uwezo wa kujiajiri baada ya kuhitimu.

Amesisitiza tamasha hilo ni endelevu na kwamba mwakani litaboreshwa huku na kwamba mwaka watatoa tuzo mbalimbali katika sanaa ya uchoraji, uigizaji na muziki.

Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Sanaa Bunifu ya chuo hicho, Dkt. Kelnony Mapana amesema idara hiyo inawasisitiza wanafunzi kufanya kazi zao kwa weledi pasipokutumia lugha za matusi na kuiga vionjo vya wasanii wa nje kwani wakifanya hivyo watapoteza uhalisia wa kazi zao.

Naye Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa nchini (Basata) Godfrey Mngereza amepongeza idara hiyo kwa kufanya tamasha hilo kwani linawejengea wanafunzi uwezo na kujiamini katika soko la ajira.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Filamu nchini, Kiago Kilonzo ameipongeza idara hiyo kwa juhudi za dhati za kutengeneza vipaji vya wanafunzi wa taaluma ya sanaa kupitia tamasha hilo.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.