Wema apelekwa gereza la Segerea

Wema apelekwa gereza la Segerea

17 June 2019 Monday 14:01
Wema apelekwa gereza la Segerea

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

MSANII wa filamu nchini Wema Sepetu amefikishwa katika gereza la Segerea Tabata jijini Dar es Salaam kuanza kutumikia kifungo cha siku saba jela.

Mapema hii leo Juni 17, 2019 mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam ilimuhukumu kutumikia siku saba jela hadi Juni 24, 2019  msanii  huyo  akisubiria uamuzi wa mahakama wa kumfutia  dhamana kutokana na kukiuka masharti

Wiki iliyopita mahakama hiyo ilifuta dhamana na  iliagiza Wema atafutwe mahala popote alipo kutokana na kutofika mahakamani kuhudhuria kesi inayomkabili

Wema ambaye aliwahi kuwa mlimbwende  'miss' Tanzania mwaka 2006 anakabiliwa na mashtaka ya kusambaza video ya ngono katika mitandao ya kijamii kupitia simu yake ya kiganjani kinyume cha sheria.

Updated: 24.06.2019 15:35
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.