Abe ataka mazungumzo kuhusu Wajapan waliotekwa Korea Kaskazini

Abe ataka mazungumzo kuhusu Wajapan waliotekwa Korea Kaskazini

14 June 2018 Thursday 17:41
Abe ataka mazungumzo kuhusu Wajapan waliotekwa Korea Kaskazini

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI ya Japan imeanza mchakato wa kutayarisha mkutano kati ya waziri mkuu Shinzo Abe na kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un baada ya kiongozi huyo wa Korea kusema yuko tayari kwa mazungumzo.

Shirika la habari la Sankei Shimbun limesema Kim alijadili uwezekano huo wakati wa mazungumzo ya kihistoria na Rais wa Marekani Donald Trump.

Japan inataka mazungumzo hayo ili kusukuma masuala muhimu ya raia wake waliotekwa na Korea Kaskazini miongo kadhaa iliyopita, hali ambayo haijaonesha hatua nzuri licha ya hatua kadhaa za kidiplomasia katika miezi ya hivi karibuni.

Abe alirudia ahadi leo ya kuanzisha mazungumzo na Korea kaskazini kuhusiana na suala hilo wakati alipokutana na familia za watu waliotekwa.

Maafisa wa serikaki ya Japan wanaangalia hali tofauti, ikiwa ni pamoja na Abe kuzuru Pyongyang mwezi Agosti mwaka huu.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.