Ajenda ya maendeleo endelevu ipo katika hatihati ikiwa…

Ripoti hiyo, “Uwekezaji na sera mpya za viwanda “, imetathimini hali ya uwekezaji duniani katika kipindi cha kati ya 2016 na 2017

Ajenda ya maendeleo endelevu ipo katika hatihati ikiwa…

Ripoti hiyo, “Uwekezaji na sera mpya za viwanda “, imetathimini hali ya uwekezaji duniani katika kipindi cha kati ya 2016 na 2017

06 June 2018 Wednesday 18:11
Ajenda ya maendeleo endelevu ipo katika hatihati ikiwa…

Na Mwandishi wetu

RIPOTI mpya ya kamati ya maendeleo na biashara ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi inaonyesha kuwa uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja (FDI) mwaka jana ulishuka kwa asilimia 23.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, uwekezaji huo ulishuka mwaka wa 2017 kutoka dola trilioni 1.87 mwaka wa 2016 hadi dola trilioni 1.43 mwaka wa 2017.

Ripoti hiyo, “Uwekezaji na sera mpya za viwanda “, imetathimini hali ya uwekezaji duniani katika kipindi cha kati ya 2016 na 2017.

Katibu Mkuu wa UNCTAD, Mukhisa Kituyi, amesema ushukaji wa FDI na pia kudorora kwa makampuni tanzu duniani vinaleta wasiwasi hususan katika nchi zinazochipukia kiuchumi.

“Ikiwa hakutafanyika juhudi za kuzuia mwenendo huu wa kupungua kwa uwekezaji wa makampuni makubwa ya kigeni katika mataifa yanayochipukia sana sana kwa miradi endelevu, matumaini yetu ya kuwa uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja (FDI) utasaidia kusukuma gurudumu la kufanikisha ajenda ya maendeleo endelevu ya 2030 yatakuwa katika hatihati,” alisema.

Uwekezaji katika sekta ya uzalishaji utahitajika mno ili kuweza kufanikisha maendeleo endelevu katika nchi maskini.

Ripoti inasema kuwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, mataifa mengi yamebadilisha sera zake za kiviwanda na kutoa mfano wa Marekani ambapo mabadiliko katika mfumo wake wa kodi, “unaweza kuathiri mpangilio wa uwekezaji duniani.”

Na hiyo ni moja ya sababu kubwa za kuporomoka kwa uwekezaji wa kigeni.

Inatoa sababu zingine zinatokana na kupungua kwa asilimia 22 ya thamani ya ubia wa makampuni yanayopatikana katika nchi tofauti na pia ununuzi wa makampuni hayo.

Isitoshe thamani ya uwekezaji wa kampuni tanzu ambazo zinatoa mwelekeo utakavyokuwa hapo baadaye nayo ilishuka kwa kiwango cha asilimia 40.

Ripoti hiyo ya UNCTAD imesema uwekezaji huo wa FDI ndiyo muhimu wa kifedha  kwa uchumi wa nchi nyingi zinazoendelea.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.