Asaad: Ni mazungumzo au nguvu itatumika kuyakomboa maeneo yetu

Alikuwa akihojiwa na kituo cha televisheni cha Russia Today

Asaad: Ni mazungumzo au nguvu itatumika kuyakomboa maeneo yetu

Alikuwa akihojiwa na kituo cha televisheni cha Russia Today

31 May 2018 Thursday 17:00
Asaad: Ni mazungumzo au nguvu itatumika kuyakomboa maeneo yetu

Na Mwandishi Wetu

SYRIA imetaka majeshi ya Marekani kuondoka nchini mwake na kuahidi kuyakomboa maeneo yote yanayodhibitiwa na waasi kupitia mazungumzo au nguvu.

Taarifa zinasema kuwa Rais Syria Bashar al Assad amesema Marekani inapaswa kujifunza kutokana na mzozo wa Iraq na kuyaondoa majeshi yake kutoka Syria, akiahidi kuyakomboa maeneo yote yanayodhibitiwa na waasi kupitia mazungumzo au nguvu.

Akizungumza katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Russia Today, Assad amesema serikali yake imeanza kufungua milango kwa ajili ya mazungumzo na kikosi cha wapiganaji cha Syrian Democratic Forces, SDF, kundi la waasi wa Kikurdi wanaoungwa mkono na Marekani linalodhibiti maeneo ya kaskazini na mashariki mwa Syria ambako majeshi ya Marekani yamekita kambi. SDF inasemekana kudhibiti thuluthi moja ya Syria.

Kiongozi huyo wa Syria amesema mazungumzo ndiyo njia ya kwanza watakayotumia, kuafikiana na kundi hilo la Kikurdi la SDF na iwapo hilo litashindikana, basi watalazimika kuyakomboa maeneo yanayodhibitiwa na SDF kwa kutumia nguvu kwani hawana budi kufanya hivyo iwe kupitia ushirikiano na Marekani au la, akiwataka Wamarekani kuondoka nchini Syria.

Ametolea mfano wa Iraq, akisema Majeshi ya Marekani yaliivamia na kuingia nchini humo bila ya kuwa na msingi wowote kisheria na sasa nchi hiyo imesalia kuwa katika mzozo.

Rais huyo wa Syria amesema watu hawatakubali wageni kuziingilia nchi za kanda hiyo ya Mashariki ya Kati tena.

Alipoulizwa na kituo hicho cha televisheni cha Russia Today kuhusu mtazamo wa Rais wa Marekani Donald Trump kuwa yeye ni mnyama, Assad amesema kile unachokisema kumhusu mtu mwingine ndivyo ulivyo.

Trump alimuita Assad mnyama baada ya shambulizi linalodaiwa kuwa la silaha za sumu katika eneo Douma mnamo mwezi uliopita.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.