China: Marekani imetangaza vita

China yaishutumu Marekani kwa kuwa ya kwanza kurusha kombora

China: Marekani imetangaza vita

China yaishutumu Marekani kwa kuwa ya kwanza kurusha kombora

15 June 2018 Friday 17:13
China: Marekani imetangaza vita

Mataifa yenye uchumi mkubwa zaidi ulimwenguni yameingia vitani kibiashara.

China imeishutumu Marekani kwa kuwa ya kwanza kurusha kombora wakati ikulu ya White House ilipothibitisha kwamba itapitisha kodi ya asilimia 25 kwa bidhaa za China zenye thamani ya dola za Kimarekani bilioni 50.

“Marekani imeendelea kubadili mawazo na sasa imeanzisha vita ya kibiashara,” Wizara ya Biashara ilisema kupitia kwa taarifa kwa vyombo vya habari.

Serikali ya China ilisema kwamba itajibu mapigo kwa kipimo kile kile cha Marekani, ambayo italenga kiasi cha bidhaa 1,100 na pia kulenga bidhaa za anga, roboti, viwandani na magari.

“China haitaki vita ya kibiashara,” taarifa hiyo ilisema, na kuongeza kwamba itajibu mapigo kulinda maslahi yake ya kitaifa, kimataifa na mfumo wa biashara ulimwenguni.

Rais wa Marekani Donald Trump kwa muda mrefu amekuwa analalamikia urari hasi wa kibiashara na China. Katika taarifa kwa vyombo vya habari Ijumaa, alisema biashara na China “imekuwa haina usawa, kwa muda mrefu sana.”

Trump alisema kodi mpya za nchi yake, ambazo zitaanza kutumika Julai 6, zina lengo la kuiadhibu China kwa wizi wa utaalamu na teknolojia ya Marekani.

CNN

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.