China ni tishio kubwa la baadae kwa Marekani – Jeshi

Korea ya Kaskazini inabaki kuwa tishio na Korea Kaskazini yenye uwezo wa kinyuklia na makombora ambayo yanaweza kufikia Marekani haikubaliki

China ni tishio kubwa la baadae kwa Marekani – Jeshi

Korea ya Kaskazini inabaki kuwa tishio na Korea Kaskazini yenye uwezo wa kinyuklia na makombora ambayo yanaweza kufikia Marekani haikubaliki

31 May 2018 Thursday 14:04
China ni tishio kubwa la baadae kwa Marekani – Jeshi

Kamanda wa Marekani ambaye anatarajiwa kuwa balozi nchini Korea Kusini anasema Korea ya Kaskazini bado ni tishio kubwa la amani katika Pasifiki lakini "ndoto ya utawala" ya China ni changamoto kubwa ya muda mrefu ya Washington.

Kamanda Harry Harris alizungumza Jumatano wakati alipokuwa anakabidhi mamlaka ya kuongoza Komandi ya Pasifiki ya Jeshi la Marekani kwa Kamanda Phil Davidson huko Pearl Harbor, Hawaii, nchini Marekani katika sherehe ambayo pia ilitangaza uhamisho wa mali za kijeshi za Marekani katika eneo hilo kwenda kwa Komandi ya India-Pasifiki.

Harris, ambaye amekuwa kiongozi wa upanuzi mkubwa zaidi kwa miaka mitatu wa Jeshi la Marekani, amerejea maneno ambayo amekuwa akiyasema mara kwa mara wakati wa uongozi wake.

"Korea ya Kaskazini inabaki kuwa tishio na Korea Kaskazini yenye uwezo wa kinyuklia na makombora ambayo yanaweza kufikia Marekani haikubaliki," alisema.

Hata hivyo aliongezea, "China bado ni changamoto kubwa zaidi ya muda mrefu. Bila kujumuisha na kushirikisha washirika wetu China itafanikiwa katika ndoto yake ya utawala huko Asia."

Akijibu maoni ya Harris Alhamisi, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Hua Chunying alisema kamanda huyo alikuwa "amejishughulisha na utawala" kwa sababu anaogopa wengine wanajaribu kuiba utawala huo kutoka kwa Marekani.

"Uwepo wa kijeshi wa Marekani katika Bahari ya Kusini ya China unazidi kwa mbali uwepo wa jumla ya China na nchi nyingine za pwani," Hua alisema, akiita shutuma za Marekani kuwa China inajitanua kijeshi "kama mwizi anayepiga kelele, 'Acha, mwizi!'"

Kupeleka kwa majeshi na ujenzi katika Bahari ya Kusini ya China ni sehemu ya kujihami kwake, Hua aliongeza.

Harris alizungumza pamoja na Waziri wa Ulinzi wa Marekani James Mattis, ambaye alisimama huko Hawaii akiwa njiani kwenda nchini Singapore kwa ajili ya mkutano wa usalama, mkutano ambao utatazama masuala yanayohusiana na Bahari ya Kusini ya China na Korea Kaskazini.

Haijulikani ni jukumu gani Harris atakuwa nalo katika mazungumzo na Pyongyang kuelekea kwenye mazungumzo kati ya Rais wa Marekani Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un huko Singapore mnamo Juni 12. Uteuzi wa Harris ulipelekwa kwa bunge la Seneti Mei 18 kabla ya uthibitisho wake.

Waziri huyo alikuwa ni chaguo la kwanza la Trump kwa kujaza nafasi ya balozi iliyo wazi nchini Australia, lakini uteuzi huo uliondolewa saa kadhaa kabla ya kuthibitishwa mwezi Aprili. Vyanzo viliiambia CNN wakati huo kwamba uamuzi huo ulikuwa ni wazo la Waziri wa Mambo ya Nje Mike Pompeo, ambaye amekuwa muhimu katika kuweka msingi kwa mkutano wa Trump na Kim.

CNN

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.