banner68
banner58

China yathibitisha kumshikiria Rais wa Interpol

China yathibitisha kumshikiria Rais wa Interpol

08 October 2018 Monday 13:18
China yathibitisha kumshikiria Rais wa Interpol

NCHI ya China imethibitisha kumzuia Rais wa Shirika la Polisi wa Kimataifa (Interpol), Meng Hongwei ikidai kuwa anafanyiwa uchunguzi na Tume ya Kupambana na Rushwa juu ya tuhuma ya ukiukaji wa sheria inayomkabili.

Wakati hayo yakijiri, taarifa zinaeleza kwamba Interpol imepokea barua ya kujiuzulu kwa Meng kutoka katika ofisi ya rais.

Meng ambaye mara ya mwisho kuonekana katika makao makuu ya Interpol mjini Lyon nchini Ufaransa akielekea China ilikuwa Septemba 25 2018, alitarajiwa kuachia madaraka katika shirika hilo mwaka 2020.

Rais huyo wa Interpol alichaguliwa kushika wadhifa huo mwezi Novemba mwaka 2016 ambaye alikuwa raia wa kwanza wa China kushikilia wadhifa huo.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.