Damu yamwagika wakati wa kuikomboa bandari muhimu, UN yaingilia kati

Waasi wa Kihouthi nchini Yemen wanaungwa mkono na Iran

Damu yamwagika wakati wa kuikomboa bandari muhimu, UN yaingilia kati

Waasi wa Kihouthi nchini Yemen wanaungwa mkono na Iran

15 June 2018 Friday 12:13
Damu yamwagika wakati wa kuikomboa bandari muhimu, UN yaingilia kati

Na Mwandishi Wetu

WATU 39 wameuawa wakati wa mapambano ya kuikomboa bandari ya muhimu ya Hoidedah huko nchini Yemeni.

Taarifa zinasema kuwa majeshi yanayounga mkono serikali nchini Yemen yameendelea na mapambano makali dhidi ya waasi ambapo idadi hiyo ya watu waliuwawa leo, wakati wakipambana na mashambulizi ya Saudi Arabia na Umoja wa falme za kiarabu.

Mapigano hayo yamekuja wakati baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likijitayarisha kufanya mazungumzo kuhusu operesheni ya kijeshi, ambayo Urusi imeonya kwamba inaweza kusababisha madhara makubwa kwa nchi nzima.

Majeshi ya Yemen yakiungwa mkono na muungano unaoongozwa na Saudi Arabia yalianzisha mashambulizi jana kuukomboa mji wa bandari wa Hodeidah, ambao umekuwa ukidhibitiwa na waasi wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran pamoja na mji mkuu wa Sanaa tangu mwaka 2014.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.