Iran yatahadharishwa kuhusu kuvuka mstari mwekundu

Le Drian amesema daima ni hatari kujaribu kuvuka mipaka iliyowekwa

Iran yatahadharishwa kuhusu kuvuka mstari mwekundu

Le Drian amesema daima ni hatari kujaribu kuvuka mipaka iliyowekwa

06 June 2018 Wednesday 17:57
Iran yatahadharishwa kuhusu kuvuka mstari mwekundu

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa mambo ya nje wa Ufaransa Lean –Yves Le Drian ametahadharisha hatari ya Iran ambayo inataka kuvuka mstari mwekundu baada ya kutoa tamko lake kuhusu uboreshaji wa madini ya urani.

Amesema tamko la Iran juu ya uboreshaji wa madini ya Uran ikiwa makubaliano ya mpango wake wa nyuklia yatasambaratika ni hatua ambayo itafikia kuuvuka "mstari mwekundu".

Le Drian amesema daima ni hatari kujaribu kuvuka mipaka iliyowekwa amesema na kuongeza kuwa mikakati ya kuyaokoa makubaliano ya mpango wa nyuklia wa Iran bado iko imara.

Iran imetoa taarifa kwa Umoja wa Mataifa juu ya mipango yake ya kuongeza kiwango cha kurutubisha madini ya Urani kulingana na makubaliano yaliyoafikiwa mnamo mwaka 2015 baina yake na mataifa makubwa ya dunia.

Iran inachukua hatua hiyo wakati ambapo pana hali ya wasiwasi juu ya mustakabali wa mkataba ya kihistoria ulioafikiwa baina yake na mataifa hayo makubwa juu ya mpango wake wa nyuklia.

Msemaji wa shirika la nishati ya nyuklia la Iran Behrouz Kamalvandi amenukuliwa na vyombo vya habari vya nchini mwake akisema kuwa Iran imewasilisha barua kwa shirika la kimataifa la nishati ya nyuklia IAEA inayofafanua juu ya hatua yake.

Hali hiyo ya wasiwasi kati ya Iran na nchi za Magharibi imezuka upya baada ya Rais wa Marekani Donald Trump mwezi uliopita kutangaza kuwa ameiondoa nchi yake kwenye makubaliano hayo yaliyofikiwa mnamo mwaka 2015.

Wakati huo huo mkurugenzi wa mpango wa nyuklia wa Iran, Ali Akbar Salehi amethibitisha kuwa nchi yake imeshaanza kazi ya kuikarabatimitambo ya kurutubishamadini ya Urani kwenye kituo chake cha Natanz.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.