Israel yajibu mapigo, ni baada ya kushambuliwa mfululizo kwa makombora leo

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, aliapa kuchukua hatua kali

Israel yajibu mapigo, ni baada ya kushambuliwa mfululizo kwa makombora leo

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, aliapa kuchukua hatua kali

29 May 2018 Tuesday 14:36
Israel yajibu mapigo, ni baada ya kushambuliwa mfululizo kwa makombora leo

Na Mwandishi Wetu

MAKOMBORA 25 yamevurumishwa kusini mwa Israel na wanamgambo wa Kipalestina jambo lililoongeza hali ya wasi wasi katika eneo la mpakani.

Imeripotiwa kuwa makombora hayo hayakuleta madhara yamerushwa na wanamgambo wa Kipalestina huko Gaza leo mapema.

Taarifa ya jeshi la Israel ilisema makombora hayo yamevurumishwa kuelekea maeneo kadhaa nchini Israel, huku mengi yakizuiwa na mfumo wa kuzuia makombora wa Iron Dome.

Polisi walisema makombora kadhaa yameanguka katika maeneo ya wazi upande wa Israel, lakini hakuna ripoti zozote za majeruhi zilizotolewa.

Jeshi lilisema makombora mengine mawili yalifyetuliwa kutokea Gaza baada ya mfululizo wa kwanza wa makombora, moja limelipuka karibu na jengo la shule ya chekechea lakini inaaminiwa hakukuwa na mtoto yeyote ndani ya jengo hilo wakati wa tukio.

Duru za usalama za Palestina zilisema vifaru vya Israel vimeyashambulia maeneo ya kufuatilia matukio ya makundi ya Hamas na Islamic Jihad karibu na mpakani.

Msemaji wa jeshi la Israel alisema hana taarifa kuhusu hujuma hiyo.

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, aliapa kuchukua hatua kali.

"Israel huchukulia kwa uzito mkubwa mashambulizi dhidi yake na jamii zake yanayofanywa na Hamas na Islamic Jihad kutokea Ukanda wa Gaza. Jeshi la Israel litajibu mashambulizi haya kwa nguvu," alisema Netanyahu wakati wa mkutano kaskazini mwa Israel.

Israel iliuteka Ukanda wa Gaza, Ukingo wa Magahribi wa mto Jordan na Jerusalem mashariki katika vita vya Mashariki ya Kati mnamo mwaka 1967.

Makazi katika Ukingo wa Magharibi sasa ni nyumbani kwa takriban Waisraeli 400,000.

Waisraeli wengine 200,000 wanaishi Jerusalem Mashariki, eneo ambalo Israel ililigawanya katika hatua ambayo haitambuliwi kimataifa.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.