Kipigo kikali kutoka Israel: Hamasi wazidiwa waomba kusitisha

Kulingana na afisa mmoja kutoka Palestina upatanisho kutoka Misri ndio umesababisha uwepo wa makubaliano ya kusitisha mapigano, ambayo hayakwenda mbali na...

Kipigo kikali kutoka Israel: Hamasi wazidiwa waomba kusitisha

Kulingana na afisa mmoja kutoka Palestina upatanisho kutoka Misri ndio umesababisha uwepo wa makubaliano ya kusitisha mapigano, ambayo hayakwenda mbali na...

31 May 2018 Thursday 10:59
Kipigo kikali kutoka Israel: Hamasi wazidiwa waomba kusitisha

Na Mwandishi Wetu

KUNDI ka Hamas limeomba kusitisha mapigano na Israel baada ya kuzidiwa huko ukanda wa Gaza ,pia kurejea makubaliano ya zamani imeripotiwa

Akizungumza Khalil al-Hayah, Naibu Mkuu wa Hamas mjini Gaza, amesema wamekubaliana kurejelea makubaliano ya zamani yaliyofikiwa ya kusimamisha mapigano. Katika taarifa yake al Hayah amesema watajitolea kusimamia makubaliano hayo ili mradi tu Israel nayo iwe na nia ya kuyaheshimu makubaliano hayo.

Kulingana na afisa mmoja kutoka Palestina upatanisho kutoka Misri ndio umesababisha uwepo wa makubaliano ya kusitisha mapigano, ambayo hayakwenda mbali na kuimarishah hali ya utulivu kwa pande zote mbili. Aidha Msemaji wa Hamas Hammad Al-Reqeb, amesema hawatakubali kushambuliwa na wako tayari kujibu iwapo hilo litafanyika

Huku hayo yakiarifiwa hii leo waziri wa elimu wa Israel Naftali Bennett, ambaye pia ni mwanachama wa Baraza la Mawaziri wa Usalama, amekanusha suala hilo akisema hakuna aina yoyote ya makubaliano kati yao na Hamas. Ameongeza kuwa hali leo ni shwari lakini itategemea ni kitu gani Hamas watakachofanya, amesema kundi hilo likivuruga hali kuwa mbaya hata wao pia wako tayari kujibu.

Awali msemaji wa jeshi la Israel, Jonathan Conricus alisema wanamgambo wa Palestina walirusha makombora na maroketi 100 nchini Israel usiku kucha huku jeshi la Israel likijibu kwa kuripua maeneo kadhaa ya kijeshi katika eneo la pwani lililozingirwa. Majibizano hayo makali yamekuja baada ya zaidi ya wapalestina 100 kuuwawa na wanajeshi wa Israel katika vurugu wakati wa maandamano wiki kadhaa zilizopita.

Jana jioni Marekani iliitisha mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kujadili juu ya mashambulizi ya maroketi kutoka Gaza. Umoja wa Ulaya nao umelaani shambulizi lililofanywa na Palestina. "Mashambulizi dhidi ya raia hayatakubalika kabisa katika hali yoyote ile," alisema msemaji wa Umoja huo Maja Kocijancic.

Azania Post

Updated: 31.05.2018 19:44
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.