Libya yakataa katakata kugeuza matumizi ya ardhi yake

Ni baada ya serikali ya Italia kukataa wakimbizi hao kupokelewa Ulaya

Libya yakataa katakata kugeuza matumizi ya ardhi yake

Ni baada ya serikali ya Italia kukataa wakimbizi hao kupokelewa Ulaya

26 June 2018 Tuesday 15:17
Libya yakataa katakata kugeuza matumizi ya ardhi yake

Na Mwandishi Wetu

ARDHI ya Libya kamwe haitatumika kuweka vituo vya mapokezi ya wahamiaji serikali ya nchi hiyo yaweka bayana.

Hivi karibuni serikali hiyo ilitakataa kata kata wazo la Waziri mpya wa mambo ya ndani wa Italia Matteo Salvini la kuwekwa vituo vya mapokezi ya wahamiaji katika ardhi yake.

Haya yanakuja huku ikiwa baadhi ya mataifa ya Umoja wa Ulaya yanaona vituo hivyo ni mojawapo ya njia za kukabiliana na wakimbizi wanaoingia Ulaya.

Katika kikao na waandishi wa habari mjini Tripoli pamoja na Salvini, naibu Waziri Mkuu wa Libya Ahmed Meitik amesema serikali yake iko tayari kufanya kazi na Umoja wa Ulaya kuhusiana na uhamiaji haramu.

Lakini Libya inapinga suala la kuwekwa kwa vituo vya mapokezi ya wakimbizi nchini mwake.

Azania Post

Keywords:
Libya
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.