Macron aichachamalia Italia kwa kuikatalia meli ya wahamiaji

Macron aichachamalia Italia kwa kuikatalia meli ya wahamiaji

13 June 2018 Wednesday 17:05
Macron aichachamalia Italia kwa kuikatalia meli ya wahamiaji

Na Mwandishi Wetu

KITENDO cha Italia kukataa kuipokea meli ya Aqurius iliyokuwa imebeba wahamiaji na wakimbizi zaidi ya 600 kimemkasirisha sana Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.

Meli hiyo kubwa na ya kisasa inamilikiwa na shirika la misaada la Kifaransa ilikuwa imebeba watu wapatao 629.

Macron ameikosoa vikali Italia kwa kukataa kuipokea meli hiyo ambayo ilikuwa na idadi tajwa ya wahamiaji na wakimbizi akisema nchi hiyo ilishindwa kutimiza wajibu wake kulingana na sheria ya kimataifa kuhusu usafiri wa baharini.

Msemaji wa rais huyo, Benjamin Grivaux alisema mwenendo wa Italia ulikuwa wa kinafiki na kutowajibika, kwa kuzingatia mazingira ya kibinadamu yaliyoihusu meli hiyo.

Grivaux alisema Rais Macron alieleza msimamo wake kuhusu hatua za Italia katika mkutano wa baraza lake la mawaziri, ambapo pia aliipongeza Uhispania kwa ahadi yake ya kuipokea meli hiyo inayomilikiwa na shirika la msaada la Ufaransa.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.