Mahasimu Sudan ya Kusini wakutana chini ya usimamizi wa IGAD

Wakutana nchini Ethiopia

Mahasimu Sudan ya Kusini wakutana chini ya usimamizi wa IGAD

Wakutana nchini Ethiopia

20 June 2018 Wednesday 15:57
Mahasimu Sudan ya Kusini wakutana chini ya usimamizi wa IGAD

Na Mwandishi Wetu

MKUTANO baina ya mahasimu wawili wa kisiasa nchini Sudan Kusini unafanyika leo huko Adis Ababa chini ya usimamizi wa IGAD

Viongozi wa pande mbili hizo watakutana ana kwa ana kwa mara ya kwanza kwa karibu miaka miwili kama sehemu ya juhudi za kujaribu kuvimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe katika taifa hilo changa zaidi duniani.

Serikali ya Ethiopia imetangaza kuwa Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar watakutana mjini Addis Ababa, kwa mualiko wa waziri mkuu wa Ethiopia.

Mkutano huo wa ana kwa ana unasimamiwa na jumuiya ya ushirikiano wa maendeleo wa nchi za Afrika Mashariki na pembe ya Afrika- IGAD, ambayo imeongoza mikutano chungu nzima ya kutafuta amani Sudan Kusini bila ya mafanikio.

Shinikizo limezidi kwa pande zinazozana Sudan Kusini kumaliza mzozo ambao umedumu tangu 2013, uliosababisha vifo vya maelfu ya watu na kuwaacha mamilioni wengine bila ya makazi au wakimbizi katika mataifa jirani.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.