Mama mjamzito akuta Panya aliyekufa kwenye supu mgahawani

Mama mjamzito akuta Panya aliyekufa kwenye supu mgahawani

14 September 2018 Friday 12:10
Mama mjamzito akuta Panya aliyekufa kwenye supu mgahawani

Migahawa maarufu nchini China imepoteza kiasi cha Dola milioni 190 katika thamani ya soko baada ya mama mmoja mjamzito kukuta panya aliyekufa kwenye supu kwenye moja ya migahawa hiyo.

Hisa za migahawa hiyo ya Hotpot imeporomoka vibaya, baada ya picha za panya huyo aliyekufa akitolewa kwenye bakuli la supu kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ambapo mgahawa wake katika Jimbo la Shandong umefungwa kwa muda.

Aidha, kwa mujibu wa mtandao wa habari wa Kankan News, mgahawa huo ulimpa mama huyo Dola za Kimarekani 729 kama fidia kufuatia tukio hilo lakini alizikataa.

Mwanamke huyo mjamzito ambaye alikwenda katika mgahawa huo pamoja na familia yake mnamo Septemba 6 alimuona panya aliyekufa wakati tayari akiwa amekula vipande kadhaa vya nyama kwenye supu.

Hata hivyo, taarifa zaidi zimesema kuwa mmoja wa wafanyakazi wa mgahawa huo alimshauri mume wa mama mjamzito atoe mimba kama ana wasiwasi kuhusu afya ya kichanga chake na kuahidi kumpa fedha kwa ajili ya kuavya mimba yake

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.