Mamia ya magaidi waliokamatwa nje sasa kurudishwa nyumbani

Mamia ya magaidi waliokamatwa nje sasa kurudishwa nyumbani

29 May 2018 Tuesday 10:47
Mamia ya magaidi waliokamatwa nje sasa kurudishwa nyumbani

Na Mwandishi Wetu

MAGAIDI 105 wa Mali waliokamatwa ughaibuni wanatarajiwa kurudishwa nchini mwao wakati wowote kuanzia sasa, maafisa wa usalama wamesema.

Taarifa zinasema kuwa Algeria itawarudisha nyumbani magaidi hao, waliokamatwa na vikosi vya kupambana na ugaidi vya Algeria katika mikoa mitano iliyo kusini mwa nchi hiyo.

Ofisa usalama aliyenukuliwa na Gazeti la El Watan la Algeria alisema, magaidi hao walikamatwa kutokana na kujenga kambi za mafunzo nchini Algeria ili kutoa mafunzo kwa kundi la wapiganaji la Mali Ansar Eddine.

Ofisa huyo amesisitiza kuwa magaidi hao wanashikiliwa na kuorodheshwa kuwa watu hatari ambao wanatakiwa kurudishwa nyumbani chini ya ulinzi mkali.

Algeria imeamua kuwarudisha watu hao mjini Bamako kwa ndege baada ya kushauriana na ubalozi wa Mali mjini Algiers.

Keywords:
MaliAlgeria
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.