Marekani yajitoa baaada ya kuona Israel ikionewa

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameupongeza uamuzi huo wa Marekani

Marekani yajitoa baaada ya kuona Israel ikionewa

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameupongeza uamuzi huo wa Marekani

20 June 2018 Wednesday 15:48
Marekani yajitoa baaada ya kuona Israel ikionewa

Na Mwandishi wetu

KITENDO cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kuwalinda wafanya maovu na kuionea Israel kimeilazimu Marekani kusitisha uanachama wake.

Taarifa zinaonyesah kuwa balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Nikki Haley ametangaza Washington imejiondoa kutoka kwa baraza hilo akiishutumu asasi hiyo ya kimataifa kwa kuwalinda wanaofanya maovu, unafiki na kuionea Israel mara kwa mara.

Haley na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo wamelishutumu baraza hilo la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu kwa muda mrefu kuwalinda wanaokiuka haki za binadamu na kuwa na upendeleo kuhusu masuala ya kisiasa.

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Federica Mogherini amesema hatua hiyo ya Marekani inaweza kuhujumu wajibu na hadhi ya nchi hiyo kimataifa.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameupongeza uamuzi huo wa Marekani.

Hatua hiyo ndiyo ya hivi punde kuchukuliwa na utawala wa Rais Donald Trump kujiondoa kutoka kwa mikataba ya kimataifa ikiwemo kujiondoa kutoka kwa makubaliano kuhusu mpango wa kinyuklia wa Iran, makubaliano ya kuyalinda mazingira yaliyofikiwa Paris na mikataba kadhaa ya kibiashara.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.