May atoa yake ya moyoni kwa Netanyahu kuhusu makubaliano ya Iran

May amesema kuwa anaunga mkono makubaliano na Iran yanayozuia nchi hiyo kupata silaha za kinyuklia

May atoa yake ya moyoni kwa Netanyahu kuhusu makubaliano ya Iran

May amesema kuwa anaunga mkono makubaliano na Iran yanayozuia nchi hiyo kupata silaha za kinyuklia

07 June 2018 Thursday 13:00
May atoa yake ya moyoni kwa Netanyahu kuhusu makubaliano ya Iran

Na Mwandishi Wetu

UINGEREZA imeeleza msimamo wake kuhusu makubaliano ya Nyuklia ya Iran, licha ya serikali ya Marekani chini ya Rais Donald Trump kujitoa.

Tayari Waziri mkuu wa Uingereza Bibi Theresa May amemwambia mwenzake wa Israel Bw. Benjamin Netanyahu kuwa London inaunga mkono kithabiti makubaliano ya nyuklia ya Iran, licha ya Marekani kujitoa kwenye makubaliano hayo.

Akizungumza na Bw. Netanyahu Bibi May amesema kutekeleza makubaliano ya nyuklia ya Iran ni njia bora ya kuizuia nchi hiyo kutengeneza silaha za nyuklia.

Mawaziri wakuu wa nchi hizo mbili pia wamekubaliana kuhusu hitaji la kuzuia shughuli za Iran za kuvuruga utulivu wa Mashariki ya Kati.

Mkutano huo umefanyika baada ya Bw. Netanyahu kufanya majadiliano kuhusu suala hili na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa na Chansela wa Ujerumani Angela Merkel, ambao wote wameeleza kuunga mkono makubaliano hayo.

Hata hivyo msemaji wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki IAEA amesema Iran imelifahamisha kuhusu mipango yake ya kuongeza uwezo wa kurutubisha madini ya uranium.

Mapema ya wiki hii kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei alitaka kufanyika kwa maandalizi ya kuongeza uwezo wa kurutubisha madini ya uranium, kama makubaliano ya nyuklia ya Iran yakivunjwa.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.