banner68
banner58

Mazoezi ya Kijeshi huenda yakasitisha mkutano wa Trump na Kim mwezi ujao

banner57

Mazoezi ya Kijeshi huenda yakasitisha mkutano wa Trump na Kim mwezi ujao

16 May 2018 Wednesday 18:15
Mazoezi ya Kijeshi huenda yakasitisha mkutano wa Trump na Kim mwezi ujao

MKUTANO baina ya Rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Korea Kaskazini Kim Jong Un uliopangwa kufanyika mwezi ujao upo katika hatihati ya kufanyika.

Kutofanyika kwa mkutano huo kunatokana na kuendelea kwa mazoezi ya kijeshi baina ya Korea Kusini na Marekani, jambo ambalo Pyongyang imekuwa ikipinga sana

Awali, Korea Kaskazini iliufuta pia mkutano wa ngazi ya juu ambao ungefanyika leo kati yake na Korea Kusini.

Onyo hilo la Korea Kaskazini limetolewa na makamu wa kwanza wa waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo, katika kipindi cha masaa kadhaa baada ya taifa hilo kusitisha ghafla mkutano wa maafisa wa ngazi ya juu na Korea Kusini, ikipinga mazoezi ya kijeshi ya pamoja kati ya Marekani na Korea Kusini, ambayo kwa muda mrefu serikali ya Pyongyang imekuwa ikidai ni maandalizi ya uvamizi.

Hatua hiyo ya kushtukiza inapoza joto la hatua zisizo za kawaida za kuridhia mazungumzo kutoka taifa hilo ambalo kwa mwaka uliopita lilikuwa likifanya mfululizo wa majaribio ya makambora,na kuzua wasiwasi kwamba eneo hilo lipo katika hatua ya kuingia vitani.

Wachambuzi wanasema sio kwamba Korea Kaskanzini inataka kupingana na hatua zote za kidiplomasia lakini inataka kunufaika katika mazungumzo hayo kati ya kiongozi Kim na Rais Trump,iliyopangwa Juni 12 huko Singapore.

Katika taarifa yake iliyotangazwa na vyombo vya habari vya umma vya nchi hiyo makamu wa kwanza wa wizara ya mambo ya nje wa Korea Kaskanzini, Kim Kye Gwan amenukuliwa akisema "Hatuna tena maslahi katika mazungumzo ambayo yanatatuweka katika wakati mgumu na kufanikisha matakwa ya upande mmoja, ambayo itatulazimisha kulizingatia pale tutakapo ridhia mkutano wa kilele kati ya Korea Kaskazini na Marekani.”

Baadhi ya wachambuzi wanasema kulizusha suala la Libya, ambayo iliiharibu mpango wake wa nyuklia katika miaka ya 2000 kwa masharti ya kupunguziwa vikwazo iliyokewa katika kipindi hicho inaweza kuhatarisha mustakabali wa mazungumzo hayo kati ya Korea Kaskazini na Marekani.

Kim Jong Un aliingia madarakani majuma kadhaa baada ya kifo cha kiongozi wa zamani wa Libya Moammar Gadhafi kilichotokea katika mikono ya vikosi vya waasi Oktoba 2011.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.