Mbunge awaonya wanawake kutojihusisha na wanaume wa rangi tofauti wakati wa kombe la dunia

Amewaonya kuwa wakifanya hivyo wanaweza kuzaa watoto wenye rangi tofauti

Mbunge awaonya wanawake kutojihusisha na wanaume wa rangi tofauti wakati wa kombe la dunia

Amewaonya kuwa wakifanya hivyo wanaweza kuzaa watoto wenye rangi tofauti

15 June 2018 Friday 11:23
Mbunge awaonya wanawake kutojihusisha na wanaume wa rangi tofauti wakati wa kombe la dunia

Na Mwandishi wetu

MBUNGE wa mmoja mwanamke nchini Urusi amewataka wanawake nchini humo kutojihusisha na uhusiano na wageni wakati huu wa kombe la dunia.

Aidha mbunge huyo machachcari Tamara Plentyova ameonya kuwa kufanya hivyo kunaweza kuleta watoto rangi tofauti.

Plentyova mkuu wa kamati ya familia, wanawake na masuala ya watoto bungeni, alisema kuwa hata iwapo uhusiano huo utasababisha kufanyika kwa harusi, wanawake au watoto wao watachukuliwa na nwanamume huyo ambaye atakuwa raia wa kigeni.

''Hata wakiolewa, watawachukua, halafu watashindwa namna ya kurudi," Bi Pletnyova alisema katika kituo cha Govorit Moskva.

"Baadaye watakuja kwangu, wasichana wakilia kwamba watoto wao wamechukuliwa''.

Alisema kuwa wanawake waliopata watoto na raia wa kigeni wakati wa michezo ya Olimpiki ya 1980 mjini Moscow walisalia kuwa wanawake wasio na wanaume.

''Ni vyema iwapo ni mtu wa rangi inayofanana na yako lakini iwapo ni mtu wa rangi tofauti basi kunakuwa na shida''.

''Ni muhimu kuwa na watoto wetu'', alisitiza Bi Pletnyova.

Warusi wenye rangi tofauti walikuwa wakiitwa 'watoto wa Olimpiki' ama 'watoto wa sherehe' baada ya Muungano wa Sovieti kuwaalika Waafrika, watu wa mashariki ya kati na raia wa Marekani kusini.

Warusi wenye ngozi nyeusi hadi leo hukabiliwa na maswali mengi ya ubaguzi wa rangi katika taifa ambapo chini ya asilimia moja ya idadi ya watu ni watu weusi.

Zaidi ya watalii milioni moja wa kigeni wanatarajiwa kuhudhuria kombe la dunia, swala linalozua wasiwasi kuhusu ubaguzi wa rangi na wapenzi wa jinsia moja hususan wakati ambapo wanachama wenye msimamo mkali wa Cossack watazuru mataifa yanayoandaa dimba hilo.

Azania Post

Updated: 15.06.2018 11:33
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.