banner58

Mdomo wamponza kamishna masuala ya bajeti

Mdomo wamponza kamishna masuala ya bajeti

30 May 2018 Wednesday 17:28
Mdomo wamponza kamishna masuala ya bajeti

Na Mwandishi Wetu

KAMISHNA wa masuala ya bajeti wa Umoja wa Ulaya Gunther Oettinger ameponzwa na matamshi yake kuhusu shinikizo la masoko.

Imeripotiwa kuwa Oettinger alisema kuwa shinikizo la masoko huenda likachangia namna upigaji kura utakavyokuwa nchini Italia, yamemsababishia matatizo.

Katika mahojiano na waandishi wa habari wa Ujerumani, Kamishna huyo alisema hana hofu kuwa uchaguzi mpya utaviimarisha vyama vya siasa za kizalendo nchini Italia - kitu ambacho wachambuzi wanasema huenda kikaifanya nchi hiyo kuondoka katika kanda ya sarafu ya euro au hata Umoja wa Ulaya.

Badala yake, anahisi kuwa masoko ya fedha na hali ya uchumi wa Italia vitawashawishi wapiga kura kutowachagua viongozi wa vyama vya kizalendo vya siasa za mrengo wa kushoto au mrengo wa kulia.

Rais wa Baraza la Ulaya Donald Tusk na Rais wa Halmashauri Kuu ya Ulaya Jean-Claude Juncker wamejitenga na matamshi hayo ya Oettinger.

Juncker amesema hatima ya Italia haiko mikononi mwa masoko ya fedha akiongeza kuwa Italia inastahili heshima. Mwanasiasa huyo wa Ujerumani ameomba radhi akisema kauli zake hazikuwa na nia ya kuikosea heshima Italia.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.