banner68
banner58

Merkel akosoa makubaliano ya Iran, asema yanafaa kuendelezwa

Merkel akosoa makubaliano ya Iran, asema yanafaa kuendelezwa

17 May 2018 Thursday 17:18
Merkel akosoa makubaliano ya Iran, asema yanafaa kuendelezwa

KIONGOZI wa Ujerumani, Angela Merkel ameukosoa mpango wa nyuklia wa Iran lakini amesema kuwa wamekubaliana kuendeleza.

Amesema kuwa nchi za Ulaya zinakubali kwamba makubaliano yana upungufu lakini inabidi kuendelezwa

Viongozi wa nchi 28 za Umoja wa Ulaya wanaokutana mji wa Sofia nchini Bulgaria, wameweka mshikamano katika kuyanusuru makubaliano hayo yaliyosainiwa mwaka 2015, baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kuiondoa nchi yake, na kurejesha vikwazo dhidi ya Iran, akilalamikia mpango wa makombora wa nchi hiyo na kujiingiza kwake katika mizozo ya Mashariki ya Kati.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron pia amesema Ulaya inafanya juhudi kuyaokoa makubaliano hayo, ili iweze kuendeleza biashara na Iran.

Tehran imetoa tahadhari kwamba inaweza kuanzisha urutubishaji wa madini ya Urani bila kikomo, ikiwa Ulaya itashindwa kuihakikishia kwamba faida zitokanazo na kuondolewa kwa vikwazo chini ya makubaliano hayo zitaendelea kupatikana.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.