Merkel hasikii, wala haambiwi kitu kuhusu mgogoro wa uhamiaji

Merkel hasikii, wala haambiwi kitu kuhusu mgogoro wa uhamiaji

17 June 2018 Sunday 11:54
Merkel hasikii, wala haambiwi kitu kuhusu mgogoro wa uhamiaji

Na Mwandishi Wetu

KANSELA wa Ujerumani, Angela Merkel bado hajakata tamaa kuhusu mgogoro wa wahamiaji haramu, na sasa anapanga kuitisha mkutano kujadili suala hilo haraka.

Imetarifiwa kuwa Merkel ataitisha mkutano maalumu na mataifa kadhaa ya Umoja wa Ulaya yanayoathiriwa na mgogoro wa uhamiaji wakati kukiwa na mvutano kati yake na waziri wa mambo ya ndani Horst Seehofer.

Mkutano huo huenda ukafanyika kabla ya mkutano wa kawaida wa kilele wa viongozi wa mataifa ya Umoja wa Ulaya uliopangiwa mwishoni mwa mwezi huu. 

Merkel anapanga kujadili suala hilo pamoja na viongozi wa mataifa yakiwemo Ugiriki, Italia na Austria, limeripoti gazeti la Bild, likinukuu vyanzo kutoka mataifa kadhaa ya Umoja wa Ulaya.

"Hadi sasa hakuna kilichoamuliwa - tuko katika awamu ya mipango," chanzo kutoka serikali ya Italia kililiambia gazeti la Bild.

"Pia bado haijajulikana wazi ni lini mkutano huo maalumu wa kilele utakapofanyika."

Haikujulikana mara moja iwapo Uhispania na mataifa ya kanda ya Balkan yatashiriki katika mkutano huo. Msemaji wa serikali ya Ujerumani hakupatikana mara moja kuzungumzia ripoti hiyo.

Msimamo wa Merkel umekuwa kutafuta suluhisho la ngazi ya Umoja wa Ulaya kuhusu uhamiaji haramu wakati wa mkutano wa kilele mjini Brussels mwishoni mwa mwezi, na ameomba kuwepo na uvumilivu.

Kwa muda mrefu, Seehorfer, veterani wa chama cha Christian Social Unioni (CSU) - ambacho ni chama ndugu na chama cha Merkel cha Christian Democratic Union (CDU) - amekuwa mwiba kwa upande wa Merkel na ametishia kumkaidi kansela na kuendelea na utekelezaji wa mipango yake siku ya Jumatatu, kuwarejeshea wahamiaji haramu mpakani mwa Ujerumani.

Katika ripoti tofauti ya Bild, alikanusha kuwa alikuwa anajaribu kuuvunja muungano wa kihafidhina. " Hakuna yeyote ndani ya CSU anataka kumpindua kansela, kuvunja ushirika wa CDU/CSU au kuvunja serikali ya muungano kati ya CDU/CSU na chama cha Social Democratic SPD," alisema Seehorfer.

"Tunataka hatimaye tupate suluhisho endelevu kwa wahamiaji waliokataliwa kutoka mipaka yetu," aliongeza.

Lengo la Seehorfer la kuzifanyia mabadiliko na kuziimarisha sheria za uhamiaji za Ujerumani linahusisha kuwakataa wahamiaji ambao tayari wamesajiliwa katika taifa lingine la Umoja wa Ulaya, wale wasio na nyaraka au wale wanaotaka kuruhusiwa kungia tena baada ya kufukuzwa.

Kansela wa Austria Sebastian Kurz akiwa na waziri Horst Seehofer. Wawili hao wana maono sawa kuhusu uhamiaji barani Ulaya.

Merkel anapinga mipango hiyo, akisema itawatwika mzigo wa wakimbizi majirani za Ujerumani na kudhoofisha mshikamano wa Umoja wa Ulaya. Katika ujumbe wa kila wiki kwa njia ya vidio siku ya Jumamosi, Merkel aliuelezea uhamiaji kama "changamoto ambayo pia inahitaji jibu la  Ulaya."

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.