banner58

Msako mkali waanzishwa kuwanasa waliochinja raia wema wapatao kumi

Hakuna mtu ambaye amekwisha kamatwa hadi sasa kwa mujibu wa msemaji huyo wa polisi Inacio Dina. Hata hivyo hakutaka kukihusisha kitendo hicho na kundi ambalo...

Msako mkali waanzishwa kuwanasa waliochinja raia wema wapatao kumi

Hakuna mtu ambaye amekwisha kamatwa hadi sasa kwa mujibu wa msemaji huyo wa polisi Inacio Dina. Hata hivyo hakutaka kukihusisha kitendo hicho na kundi ambalo...

31 May 2018 Thursday 10:49
Msako mkali waanzishwa kuwanasa  waliochinja raia wema wapatao kumi

Na Mwandishi Wetu

UHALIFU wa kinyama dhidi ya binadamu umeripotiwa huko Kaskazini mwa Msumbiji ambapo watu kumi wameuwa kwa kukatwa shingo.

Polisi wamesema kuwa watu 10 wamechinjwa na kundi la watu wenye silaha katika jimbo la kaskazini mwa nchi hiyo la Cabo Delgado, eneo ambalo mashambulizi ya Waislamu wenye itikadi kali yaliwahi kuripotiwa.

Vijana wawili wa kiume ni miongoni mwa wale waliokatwa shingo zao siku ya Jumapili, msemaji wa polisi ya Msumbiji Inacio Dina aliwaambia waandishi habari , na kuongeza kwamba sasa wameanzisha msako kuwatafuta waliohusika. Dina alithibitisha kwamba kuna watu kutoka nje ya nchi pamoja na raia wa Msumbiji katika kundi hilo la washambuliaji.

"Hili ni kundi ambalo kwa kiasi kikubwa ni dhaifu. Kile tulichokishuhudia ni kukata tamaa kwa kiasi kikubwa kwa kundi hili kwa kujaribu baadhi ya viongozi wa kundi hili kufanya uhalifu huu wa kinyama."

Hakuna mtu ambaye amekwisha kamatwa hadi sasa kwa mujibu wa msemaji huyo wa polisi Inacio Dina. Hata hivyo hakutaka kukihusisha kitendo hicho na kundi ambalo liliwauwa zaidi ya watu 20 katika jimbo la Cabo Delgado mwezi Oktoba, ama iwapo kuna uhusiano na kundi la Waislamu wenye itikadi kali. Ripoti kutoka katika eneo hilo zinazungumzia kwamba washambuliaji wana mahusano na makundi ya itikadi kali ya Kiislamu.

Msumbiji ambayo kwa kiasi kikubwa ina waumini wengi wa Kikristo , katika pwani ya kusini mashariki mwa bara la Afrika hakujakuwa na makundi ya waislamu wenye itikadi kali hapo kabla.

Mapema mwaka huu , taarifa moja katika tovuti ya kituo cha kukusanya mawazo kilicho na makao yake makuu nchini Marekani cha Kituo cha Afrika cha mitaala ya mikakati kimesema shambulio la Oktoba , liliwapata "wachunguzi wa mapambano ya wapiganaji wa kimataifa wa jihadi kwa mshangao."

Jimbo la Cabo Delgado limeshuhudia mashambulizi kadhaa yaliyofanywa na wanaoshukiwa kuwa Waislamu wenye itikadi kali tangu mwezi Oktoba mwaka jana. Mmoja kati ya wahanga katika shambulio la hivi karibuni alikuwa kiongozi wa kijiji cha Monjane, mkaazi wa eneo hilo , bila ya kutaja jina lake kwa hofu ya kulipiziwa kisasi.

Azania Post

Updated: 31.05.2018 12:48
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.