banner58

Mwanahabari auawa kwa kupigwa risasi kwa kuipinga serikali

Mwandishi huyo alifariki dunia wakati akipelekwa hospitali

Mwanahabari auawa kwa kupigwa risasi kwa kuipinga serikali

Mwandishi huyo alifariki dunia wakati akipelekwa hospitali

30 May 2018 Wednesday 17:22
Mwanahabari auawa kwa kupigwa risasi kwa kuipinga serikali

Na Mwandishi Wetu

ARKADY Babchenko ambaye ni mwandishi wa habari huko Urusi ameuwa baada ya kupigwa risasi ya mgongoni kutokana na kitendo cha kuikosoa serikali.

Imeripotiwa kuwa mwandishi huyo aliyekuwa mkosoaji mkubwa wa kile alichokiita kuwa ni vitendo vya uchokozi vinavyofanywa na Urusi nchini Georgia, Crimea, Mashariki mwa Ukraine na Syria, alipigwa risasi jana nyumbani kwake mjini Kiev.

Babchenko alifariki dunia wakati akipelekwa hospitali.

Polisi ya Ukraine imesema mke wake alimkuta akiwa chumbani akivuja damu.

Mwandishi huyo aliyekuwa na umri wa miaka 41, aliondoka Urusi mwaka wa 2017, akikabiliwa na miito ya kupokonywa uraia na kuongezeka kwa vitisho dhidi yake kutokana na maoni yake kuhusu ajali ya ndege ya Desemba 2016 ambayo iliwauwa waimbaji wa kwaya ya jeshi la Urusi waliokuwa njiani kwenda Syria kuwatumbuiza marubani wa jeshi.

Alituhumiwa kwa kukosa uzalendo, kitu alichosema kuwa kinashangaza ikizingatiwa kuwa aliipigania nchi yake katika vita vya kwanza ya kutaka kujitenga nchini Chechnya katika miaka ya 1990.

Wanasiasa wanaoiunga mkono serikali walianza kumkana na kutaka afungwe jela kutokana na maoni yake.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.