Nchi tano zenye amani zaidi duniani zatajwa, migogoro yatafuna matrililioni ya fedha

Newzealand na Iceland zinatajwa kuwa miongoni mwa mataifa yenye amani zaidi duniani

Nchi tano zenye amani zaidi duniani zatajwa, migogoro yatafuna matrililioni ya fedha

Newzealand na Iceland zinatajwa kuwa miongoni mwa mataifa yenye amani zaidi duniani

06 June 2018 Wednesday 15:31
Nchi tano zenye amani zaidi duniani zatajwa, migogoro yatafuna matrililioni ya fedha

Na Mwandishi Wetu

MIGOGORO inayoendelea barani Afrika na Mashariki ya Kati imegharimu uchumi wa dunia kiasi cha dola trilioni moja, taasisi ya uchumi na amani imesema.

Mbali ya kiasi hicho kikubwa cha fedha kupotea, utafiti unaonesha kwamba amani imepungua katika nchi nyingi duniani kufuatia migogoro inayoendelea na kusababisha wimbi kubwa la wakimbizi.

Amani duniani imepungua ikilinganishwa na hali ilivyokuwa muongo mmoja uliopita.

Sababu kubwa ya kushuhudiwa hali hiyo ni migogoro inayoendelea Mashariki ya kati na barani Afrika ambayo imeugharimu uchumi wa dunia dola trillioni kadhaa.

Mkuu wa taasisi ya uchumi na amani (IEP) yenye makao makuu yake nchini Australia, Steve Kilelea anasema kwamba amani duniani imekuwa ikipungua taratibu kwa kipindi cha muongo mmoja na kinachochangia hali hiyo ni migogoro Mashariki ya kati, na Afrika ya kaskazini ambayo athari zake zimevuka mipaka na kuingia kwenye maeneo mengine ya dunia.

Ulaya imekabiliwa na mgogoro mkubwa wa wakimbizi tangu mwaka 2015 kufuatia vita nchini Libya na Syria.

Zaidi ya watu millioni 1 kutoka Afrika na Mashariki ya kati pamoja na kutokea Afghanistan wamejaribu kufika barani Ulaya kupitia Uturuki au kupitia njia ya bahari.

Taasisi hiyo ikitumia data za taasisi za utafiti na vyuo vikuu kutoa uchambuzi wake inakadiria kwamba vurugu zilizotokea katika mwaka 2017 katika maeneo mbali mbali ya dunia zimeugharimu uchumi dola trilioni 14.8 ikiwa ni sawa na mtu mmoja kupoteza kiasi dola 2000.

Endapo nchi ambazo hazina usalama kama vile Syria, Sudan Kusini, na Iraq zingekuwa na utulivu katika hali ilivyo katika nchi zenye amani kama vile Iceland na New Zealand ina maana kila mmoja uchumi wake ungeongezeka kwa dolla 2000.

Kilelea anasema huo ndio utafiti pekee uliofanywa ambao unapima athari za vita katika uchumi wa dunia.

Ulaya imeorodheshwa kama eneo lenye utulivu zaidi duniani wakati Mashariki ya Kati na Afrika ya Kaskazini yakitajwa kuwa maeneo yenye usalama mdogo.

Nchi tano zimetajwa kuwa na amani zaidi ni Newzealand, Iceland, Austria, Portugal, na Denmark.

Ujerumani bado hali haijabadilika ikiwa katika nafasi ya 17, lakini pia kati ya nchi 36 za Ulaya nchi 23 zimetajwa kwamba hali imekuwa mbaya katika kipindi cha mwaka uliopita.

Umoja wa Mataifa mnamo mwezi Mei ulisema kwamba mgogoro wa kibinadamu nchini Syria umeongezeka mwaka huu kuliko ilivyowahi kushuhudiwa wakati mwingine wowote wa vita nchini humo ambavyo vimedumu miaka 7.

Katika nchi jirani ya Iraq kundi linalojiita dola la kiislamu linasababisha kitisho kikubwa katika mpaka ya Syria licha ya kwamba nchi hiyo ilitangaza ushindi wa mwisho mnamo mwezi Desemba dhidi ya wapiganaji hao wa itikadi kali waliokuwa wakiithibiti thuluthi moja ya Iraq.

Nchi 104 zimepunguza asilimia ya pato jumla la nchi zao ya fedha zinazotumika katika bajeti ya kijeshi wakati nchi 115 zimepunguza idadi ya wanajeshi.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.