Nchi zinazoongoza kwa vitisho, mizozo pia umasikini duniani zatajwa

Nchi zinazoongoza kwa vitisho, mizozo pia umasikini duniani zatajwa

31 May 2018 Thursday 17:53
Nchi zinazoongoza kwa vitisho, mizozo pia umasikini duniani zatajwa

Na Mwandishi Wetu

SHIRIKA la Save the Children limetoa orodha ya nchi ambazo watoto wanakabiliwa na vitisho vya mizozo, umasikini na ubaguzi wa kijinsia.

Taarifa iliyotolewa na shirika hilo la kuteta haki za watoto limesema zaidi ya nusu yao duniani wanakabiliwa na vitisho vya na mizozo, umaskini au ubaguzi wa kijinsia.

Ripoti hiyo iliyotolewa jana imeziorodhesha nchi 175 ambazo ni kitisho kwa misingi ya kuwa na ajira za watoto, kuwakosesha elimu, ndoa za utotoni pamoja na mimba za mapema.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, nane kati ya nchi 10 ambazo zimeorodheshwa kuwa mbaya zaidi kwa watoto, ziko magharibi na katikati mwa bara la Afrika, huku kitisho kikubwa kikiwa Niger.

Singapore na Slovenia zimeorodheshwa kama nchi ambazo zina kiwango cha chini cha matatizo kama hayo.

Zaidi ya watoto bilioni moja wanaishi kwenye nchi zinazokumbwa na umaskini na watoto milioni 240 wanaishi katika nchi zilizoathirika na mizozo.

Kiasi ya nchi 20 ikiwemo Sudan Kusini, Somalia, Yemen na Afghanistan, watoto 153 wanaishi katika vitisho vyote vitatu.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.