Netanyahu achachamaa, Hamas kukiona

Netanyahu achachamaa, Hamas kukiona

29 May 2018 Tuesday 14:26
Netanyahu achachamaa, Hamas kukiona

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu aliapa Jumanne kujibu "kwa nguvu kubwa" mashambulizi ya maroketi zaidi ya 25 ambazo yalirushwa asubuhi huko kusini mwa Israeli, moja likitua karibu na shule ya chekechea muda mfupi kabla ya watoto kufika.

"Israeli inatazama kwa umakini mkubwa mashambulizi hayo dhidi ya watu wake yaliyofanywa na Hamas na Islamic Jihad kutoka Ukanda wa Gaza," Netanyahu alisema wakati wa mkutano katika mkoa wa Galilaya, kabla ya mashauriano ya usalama yanayotarajiwa kufanyika baadaye leo.

"Jeshi la Israel litalipa kisasi kwa nguvu kubwa dhidi ya mashambulizi haya," waziri mkuu aliongeza.

"Israeli itamfanya mtu yeyote anayejaribu kuiumiza alipe gharama kubwa, na tunaitazama Hamas akiwajibika kwa kuzuia mashambulizi hayo dhidi yetu."

Kama suala la sera, jeshi la Israeli linaiona Hamas, ambayo inatawala Gaza, kuwa na kuwajibika kwa shambulio lolote linaloweza kutoka katika eneo hilo.

Netanyahu pia aliweka alama kwenye ukurasa wake wa Twitter akisema kuwa "makombora 57" yalivurumishwa Jumanne asubuhi, idadi kubwa sana kuliko ile iliyoelezwa na jesh na mamlaka za mitaa.

Waziri wa Ulinzi Avigdor Liberman aliita "tathmini maalumu ya hali" katika makao makuu ya jeshi huko Tel Aviv na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Israel Gadi Eisenkot na maafisa wengine wa ngazi za juu kutoka kwa huduma za kiusalama za Israeli, ofisi yake ilisema.

Mashambulizi, ambayo yalisababisha duru tatu za ving’ola katika mikoa ya Sha'ar Hanegev na Eshkol, inaonekana kufanywa na kundi la kigaidi la Islamic Jihad la Iran, kwa ajili ya kisasi kutokana na jeshi la Israel kuua wanachama wake watatu katika kutupiana risasi mpakani mapema wiki hii.

Haya ni mashambulizi makubwa kutoka Ukanda wa Gaza, kwa mujibu wa idadi ya maroketi yaliyorushwa, tangu vita ya 2014, inayojulikana katika Israeli kama Operation Protective Edge.

Idadi kuwa ya maroketi yalidunguliwa na mfumo wa ulinzi wa makombora wa Iron Dome.

"Hakuna nchi inaweza au inapaswa kukubali vitisho dhidi ya raia wake. Hata sisi hatukubali," msemaji wa Wizara ya Nje alisema.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.