Papa Francis aguswa na matatizo, changamoto za wanawake duniani

Shirikisho hilo la Vyama vya Wanawake Wakatoliki Duniani, limemwandikia Baba Mtakatifu Francisko barua ya wazi

Papa Francis aguswa na matatizo, changamoto za wanawake duniani

Shirikisho hilo la Vyama vya Wanawake Wakatoliki Duniani, limemwandikia Baba Mtakatifu Francisko barua ya wazi

31 May 2018 Thursday 18:03
Papa Francis aguswa na matatizo, changamoto za wanawake duniani

Na Mwandishi Wetu

KIONGOZI wa Kanisa katoliki duniani, Papa Francis ameonesha kuguswa na matatizo na changamoto zinazowakabili wanawake duniani, taarifa ya shirikisho iliyotolewa leo huko Vatican imesema.

Shirikisho hilo la Vyama vya Wanawake Wakatoliki Duniani, limemwandikia Baba Mtakatifu Francisko barua ya wazi, kumshukuru na kumpongeza kwa uongozi imara na thabiti, kwa ajili ya ustawi, mafao na maendeleo ya watu wote wa Mungu.

Lakini zaidi linamshukuru kwa kuguswa na mahangaiko ya watu, changamoto na magumu wanayokabiliana nayo kila kukicha.

Linampongeza kwa moyo wake wa upendo, huruma na furaha inayomwilishwa katika imani na kwamba, wao kama wanawake Wakatoliki wanapenda kumuunga mkono yeye pamoja na viongozi wote wa Kanisa katika maisha na utume wa Kanisa, ili kujenga ulimwengu unaojikita katika haki na maendeleo endelevu!

Wanawake Wakatoliki wanapenda kumpongeza Baba Mtakatifu kwa kuwashirikisha kikamilifu katika maisha na utume wa Kanisa.

Baba Mtakatifu ameonesha kuguswa sana na matatizo na changamoto zinazowakabili wanawake sehemu mbali mbali za dunia hasa kulinda na kudumisha Injili ya uhai dhidi ya utamaduni wa kifo.

Kumbe, ni wajibu wa wanawake pia kusimama kidete kulinda na kudumisha utu na heshima ya binadamu; kusaidiana na kukamilishana katika maisha na utume wa Kanisa.

Wanawawake wanapaswa kuhusishwa kikamilifu katika mchakato wa majadiliano, ili waweze kuchangia ustawi na mafao ya wengi, kwa kuwapatia wanawake nafasi ya kutumua karama na mapaji yao.

Wanawake Wakatoliki wanasema, umefika wakati wa kumwilishwa mawazo katika uhalisia wa maisha ya watu badala ya watu kuendelea “kuning’inia kwenye ombwe. Wanawake washirikishwe kikamilifu katika maisha na utume wa Kanisa.

Wanampongeza Baba Mtakatifu ambaye katika Wosia wake wa kitume, “Amoris laetitia” yaani “Furaha ya upendo ndani ya familia” anakazia umuhimu wa majadiliano katika maisha ya ndoa na familia ili kukuza na kudumisha upendo ndani ya familia.

Majadiliano yajikite katika ukweli na uwazi; kwa kusali na kutafakari; kwa kukazia mambo msingi katika maisha, ili kukuza na kudumisha Injili ya familia.

Wanawake Wakatoliki wanahamasishwa kushiriki kikamilifu katika mchakato wa majadiliano, kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya familia ya Mungu.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.