Pendekezo jipya la Trump kuunda jeshi la anga za juu lapokelewa kwa hisia tofauti

Pendekezo jipya la Trump kuunda jeshi la anga za juu lapokelewa kwa hisia tofauti

19 June 2018 Tuesday 15:54
Pendekezo jipya la Trump kuunda jeshi la anga za juu lapokelewa kwa hisia tofauti

Na Mwandishi Wetu

RAIS Donald Trump wa Marekani jana ameitaka wizara ya ulinzi ya nchi hiyo ianze mara moja kuunda jeshi la anga za juu.

Kiongozi huyo wa ngazi za juu wa Marekani amesema, uhusiano kati ya jeshi la anga na jeshi la anga za juu ni "kujitenga na usawa".

Pendekezo hilo limeungwa mkono na baadhi ya wabunge, huku watunga sheria wengine wakiwa na wasiwasi kuhusu pendekezo hilo.

Rais Trump amesema, hatma ya Marekani nje ya dunia si kama tu ni suala la utambulisho wa taifa, bali pia ni suala la usalama wa taifa.

Amesisitiza kuwa ili kujilinda, Marekani lazima ichukue nafasi ya uongozi kwenye anga ya juu.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.