Piga nikupige yaanzishwa kukomboa mji wa bandari ulio chini ya waasi

Operesheni inatarajiwa kuongozwa na Saudi Arabia

Piga nikupige yaanzishwa kukomboa mji wa bandari ulio chini ya waasi

Operesheni inatarajiwa kuongozwa na Saudi Arabia

13 June 2018 Wednesday 16:18
Piga nikupige yaanzishwa kukomboa mji wa bandari ulio chini ya waasi

Na Mwandishi Wetu

MAPIGANO makali yameanza kuukamata mji wa bandari wa Hodeidah ambao uko chini ya utawala wa waasi wa Kihouthi nchini Yemen.

Inataarifiwa kuwa vikosi vinanyoungwa mkono na muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia vimeanzisha mashambulizi yenye lengo la kuukamata mji huo.

Mashambulizi ya kuikomboa Hodeidah yanatarajiwa kuwa makali zaidi tangu vikosi vinavyoongozwa na Saudi Arabia vilipoingilia kati nchini Yemen

Tangazo la kuanza kwa operesheni hiyo kubwa limetolewa na serikali ya Yemen inayoishi uhamishoni nchini Saudi Arabia, ikisema vikosi vya ardhini vimenza kuukomboa mji wa Hodeidah, vikisaidia na ndege pamoja na meli za kivita.

Operesheni hiyo iliyopachikwa jina la ''ushindi wa dhahabu'' imeanzishwa baada ya muda wa mwisho uliotolewa na Umoja wa Falme za Kiarabu, kwa waasi wa Kihouthi kuwa wameuachia mji huo ulio kwenye Bahari ya Sham, kupita usiku wa kuamkia leo.

Bandari ya Hodeidah ni njia muhimu ya kupitishia msaada wa kibinadamu kuelekea katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran.

Keywords:
Yemen
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.