banner58

Polisi washambuliwa, wapigwa mateke kwa sababu ya chakula cha jioni

Ni nchini Ujerumani katika jiji la Dresden

Polisi washambuliwa, wapigwa mateke kwa sababu ya chakula cha jioni

Ni nchini Ujerumani katika jiji la Dresden

29 May 2018 Tuesday 15:10
Polisi washambuliwa, wapigwa mateke kwa sababu ya chakula cha jioni

Na Mwandishi Wetu

ASKARI polisi kadhaa wameshambuliwa na wakimbizi waliokuwa wanazozana kuhusu chakula cha jioni juzi katika mji wa mashariki wa Ujerumani wa Dresden.

Imeripotiwa kuwa karibu wakimbizi 50 waliwashambulia polisi baada ya kujaribu kuzuia mapambano katika kituo kimoja cha wahamiaji katika mji huo.

Maafisa wamesema polisi waliitwa baada ya walinzi wa usalama kushindwa kuzuia mabishano yaliyozuka kati ya wahamiaji wawili kutoka Georgia kuhusu chakula Ijumaa jioni.

Taarifa kutoka polisi ya Dresden imesema kisha wahamiaji 50 wakakusanyika na kuwashambulia polisi kwa kuwarushia sigara zilizowashwa moto na kuwapiga mateke.

Polisi wawili na mlinzi mmoja wa usalama walijeruhiwa wakati wa tukio hilo. Polisi zaidi waliitwa ili kuidhibiti hali hiyo.

Washukiwa wanne - wote raia wa Georgia wenye umri wa miaka 17, 20, 27 na 42 - walizuiliwa Ijumaa kwa kuvuruga amani.

Polisi imesema mmoja wao alitakiwa kurejeshwa nyumbani wakati wengine watatu wakipelekwa jela

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.