Polisi wawili wa kike wauawa kwa silaha zao wenyewe

Mtu huyo kisha alizidiwa nguvu na maafisa wa polisi na kuuawa kwa kupigwa risasi

Polisi wawili wa kike wauawa kwa silaha zao wenyewe

Mtu huyo kisha alizidiwa nguvu na maafisa wa polisi na kuuawa kwa kupigwa risasi

30 May 2018 Wednesday 16:12
Polisi wawili wa kike wauawa kwa silaha zao wenyewe

Na Mwandishi Wetu

SHAMBULIZI linalohusishwa na ugaidi limetokea leo huko Ubelgiji ambapo polisi wawili wameuawa kwa kutumia silaha zao wenyewe.

Imeripotiwa kuwa mtu aliyekuwa na silaha alifanya shambulizi linalodaiwa kuwa la kigaidi nchini Ubelgiji, kwa kuwapiga risasi na kuwaua polisi wawili wanawake akitumia bastola zao wenyewe kabla ya kumuua mpita njia. 

Ubelgiji ni nchi ambayo mchezaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta anachezea mpira.

Mtu huyo kisha alizidiwa nguvu na maafisa wa polisi na kuuawa kwa kupigwa risasi.

Waendesha mashitaka wamesema shambulizi hilo lilitokea jana katika mji wa kiviwanda wa mashariki wa Liege wakati mshambuliaji aliyekuwa na kisu alipowachoma kisu mara kadhaa polisi hao wawili wanawake kabla ya kutumia bastola zao na kuwauwa.

Ubelgiji inabaki katika hali ya tahadhari kubwa baada ya wimbi la mashambulizi yakiwemo ya mabomu ya kujitoa muhanga mjini Brussels mwaka wa 2016 ambayo yalidaiwa kufanywa na kundi linalojiita Dola la Kiislamu.

Waziri Mkuu Charles Michel alikiri kuwa mshambuliaji huyo ambaye alikuwa amepewa ruhusa ya kutoka jela kwa saa.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.