Putin ahojiwa kwa mara ya kwanza katika ikulu ya Kremlin

Uhusiano wa China na Urusi umeimarika baada ya uhasama wa muda mrefu wa enzi za Jamhuri ya Kisovieti

Putin ahojiwa kwa mara ya kwanza katika ikulu ya Kremlin

Uhusiano wa China na Urusi umeimarika baada ya uhasama wa muda mrefu wa enzi za Jamhuri ya Kisovieti

06 June 2018 Wednesday 12:20
Putin ahojiwa kwa mara ya kwanza katika ikulu ya Kremlin

Na Mwandishi Wetu

RAIS wa Urusi Vladimir Putin amehojiwa kwa mara ya kwanza na mkuu wa kituo cha radio na televisheni cha China, Bw Shen Haixiong katika ikulu ya Kremlin.

Mahojiano hayo yamefanyika siku chache kabla ya Rais huyo kufunga safari ya kwenda China kuhudhuria Mkutano wa kilele wa Baraza la viongozi wa nchi wanachama wa Shirika la ushirikiano wa Shanghai SCO na kufanya ziara ya kitaifa nchini humo.

"Mheshimiwa Rais Putin, nakushukuru kukubali kufanyiwa mahojiano maalum na Kituo Kikuu cha Radio na Televisheni cha Taifa cha China…"

Hii ni mara ya kwanza kwa rais Putin kukubali kufanyiwa mahojiano na vyombo vya habari vya nchi za nje tangu aapishwe kuwa rais wa Urusi kwa muhula mwingine, pia ni mara ya kwanza kwake kufanyiwa mahojiano na vyombo vya habari vya China kwenye Ikulu ya Kremlin.

Kabla ya kuanza kwa mahojiano hayo, Rais Putin ametoa salamu kwa watu wa China, akiitakia kila familia ya Wachina furaha na neema!

Kwenye mahojiano hayo, Rais Putin amesema Urusi inatilia maanani uhusiano wa kiwenzi na kirafiki kati yake na China, na nchi hizo mbili zimejenga uhusiano imara na wa kipekee kwenye msingi wa kunufaishana.

Amesema Mkataba wa ushirikiano wa ujirani mwema uliosainiwa mwaka 2001 kati ya Urusi  na China umeweka msingi imara kwa maendeleo makubwa yaliyopatikana kwenye uhusiano kati ya nchi hizo mbili, na maoni mengi ya pamoja ya nchi hizo mbili kuhusu namna ya kuendeleza nchi na namna ya kuwatendea wananchi, yanaziunganisha nchi hizo mbili. Rais Putin anasema:

"Tukinukuu hotuba aliyoitoa Rais Xi Jinping kwenye Mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China, ni mambo gani yana umuhimu mkubwa zaidi? Kama rais Xi alivyosema ni kuinua kiwango cha maisha ya watu. Kuna njia nyingi zinazoweza kutimiza lengo hilo, lakini lengo lenyewe ni la pamoja.

Nchini Urusi, hakuna lengo lingine licha ya kuinua kiwango cha maisha ya wananchi wetu. ndiyo maana, tunafikiria kwa makini jinsi tutakavyojenga uhusiano kati yetu na China, namna ya kutimiza malengo hayo huku tukihakikisha usalama, na kuimarisha ujenzi wa uchumi wa aina mpya kupitia uvumbuzi, teknolojia za kisasa, masikilizano ya jamii na usimamizi wa kiuchumi. Naamini kuwa tukifanya juhudi kubwa hakika tutapata mafanikio mapya. "

Kwenye mahojiano, rais Putin amesifu pendekezo la "Ukanda mmoja na Njia moja" lililotolewa na Rais Xi Jinping, na kuona ni pendekezo muhimu lenye manufaa na mustakbali.

Amesisitiza kuwa Russia siku zote inaunga mkono pendekezo hilo, na mchakato wa kuunganisha mikakati ya maendeleo ya Russia na China utapanua zaidi mustakbali wa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Mwaka jana, thamani ya biashara kati ya China na Russia iliongezeka na kufikia dola za kimarekani bilioni 87, na Rais Putin anaona ongezeko hilo ni la kuridhisha, na mwelekeo huu unapaswa kudumishwa katika siku zijazo.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.