Rais, Jaji Mkuu wa zamani waswekwa jela kwa kosa moja

Alihukumiwa jana na mahakama kuu nchini Maldives

Rais, Jaji Mkuu wa zamani waswekwa jela kwa kosa moja

Alihukumiwa jana na mahakama kuu nchini Maldives

15 June 2018 Friday 12:36
Rais, Jaji Mkuu wa zamani waswekwa jela kwa kosa moja

Na Mwandishi Wetu

RAIS wa zamani wa Maldives Maumoon Abdul Gayoom amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja na miezi saba gerezani kwa kosa la kupindisha sheria.

Kiongozi huyo alihukumiwa jana na Mahakama nchini humo ambapo ataanza kutumikia kifungo chake hivi karibuni.

Mahakama hiyo pia imemhukumu jaji mkuu wa Mahakama Kuu ya Maldives Abdulla Saeed na jaji Abdullah Yameen kifungo cha miezi 19 kwa kosa hilohilo.

Watu hao walipokamatwa na polisi, walikataa kukabidhi simu zao. Gayoom amesema idara ya uendesha mashtaka haiwezi kuthibitisha kuwa upo ushahidi wa kutosha kwenye simu zao.

Habari nyingine zinasema, watatu hao bado wanakabiliwa na kesi ya uhalifu wa kupindua serikali.

Azania Post

Updated: 15.06.2018 12:41
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.