Rais Korea Kaskazini kufanya ziara nchini Marekani ikiwa…

Rais Korea Kaskazini kufanya ziara nchini Marekani ikiwa…

08 June 2018 Friday 15:48
Rais Korea Kaskazini kufanya ziara nchini Marekani ikiwa…

Na Mwandishi Wetu

KUNA dalili ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un kufanya ziara nchini Marekani lakini itategemea mazungumzo kati yake na Rais Donald Trump yatakwenda vizuri.

Rais Donald Trump wa Marekani amesema anapenda kumwalika kiongozi mkuu wa Korea Kaskazini Kim Jong Un kufanya ziara nchini Marekani, kama mazungumzo kati yao nchini Singapore yatafanyika vizuri.

Rais Trump aliyasema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari baada ya kukutana na waziri mkuu wa Japan Bw. Shinzo Abe.

Rais Trump amesema anatumai kuwa uhusiano kati ya Marekani na Korea Kaskazini utarudi kwenye njia ya kawaida, na masuala yote yanayofuatiliwa na pande mbili yatatatuliwa.

Habari nyingine zinasema, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo amesema baada ya mazungumzo kati ya wakuu wa Marekani na Korea Kaskazini tarehe 12 Juni, atafanya ziara nchini Korea Kusini na China kuziarifu nchi hizo kuhusu hali ya mazungumzo hayo.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.