Rais wa Ufaransa atakiwa kuomba radhi kwa matamshi yake

Rais wa Ufaransa atakiwa kuomba radhi kwa matamshi yake

15 June 2018 Friday 10:32
Rais wa Ufaransa atakiwa kuomba radhi kwa matamshi yake

Na Mwandishi Wetu

NAIBU waziri mkuu wa Italia Luigi Di Maio amemtaka Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kuomba radhi kwa matamshi yake dhidi ya wahamiaji.

Wakati akitakiwa kufanya hivyo imesemwa kuwa Waziri mkuu wa Italia Giuseppe Conte amethibitisha mipango yake ya kukutana na Rais Macron siku ya leo 

Hayo yameelezwa katika taarifa, baada ya mazungumzo ya maridhiano kwa simu kati ya wanasiasa hao wawili.

Hapo mapema naibu waziri mkuu wa Italia Luigi Di Maio alisema kwamba bado anamtarajia rais Macron aombe radhi kwa matamshi yake makali aliyotoa juu ya sera za uhamiaji za Italia siku mbili zilizopita.

Macron alisema Italia imechukua hatua za dharau na kushindwa kuwajibika kwa kuzuwia meli ya wahamiaji isifunge gati nchini humo mapema wiki hii, hali iliyozusha mvutano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili, ambapo waziri mkuu Conte akitafakari kufuta mkutano unaotarajiwa kufanyika  kati yake na Macron.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.