Shemeji wa Mfalme matatani kwa ukwepaji wa kodi

Atatumikia kifungo jela

Shemeji wa Mfalme matatani kwa ukwepaji wa kodi

Atatumikia kifungo jela

13 June 2018 Wednesday 15:28
Shemeji wa Mfalme matatani kwa ukwepaji wa kodi

Na Mwandishi Wetu

SHEMEJI wa Mfalme Filipe wa Hispania ajulikanaye kama Inaki Urdangarin ataanza kutumikia kifungo cha zaidi ya miaka mitano, baada ya mahakama kumkuta na hatia ya wizi wa fedha.

Taarifa zinaonyesha kuwa mahakama ya juu ya Uhispania imeunga mkono hukumu iliyotolewa na mahakama ya chini dhidi ya mumewe mwanamfalme Cristina ya kifungo cha takriban miaka sita jela ingawa imepunguza kifungo hicho kwa miezi mitano.

Mahakama ya juu ilitowa uamuzi wake kuhusu rufaa kwamba Urdangarin ana hatia ya kuhusika na wizi wa fedha na ukwepaji kodi miongoni mwa uhalifu mwingine lakini mahakama hiyo imemfutia kosa la uhalifu wa kughushi nyaraka.

Mahakama ndogo ya Palma de Mallorca ilimhukumu Urdangarin katika kesi iliyoanza 2016 ya kutumia vibaya fedha za umma, kutumia vibaya madaraka wizi na ukwepaji kodi pamoja na kutumia ushawishi wake.

Kadhalika mahakama ya juu imeunga mkono hukumu iliyotolewa kwamba Princes Cristina alinufaika kutokana na uhalifu uliofanywa na mumewe.

Mahakama ndogo ya Marllorca sasa itatowa uamuzi wa lini Urdangarin ataanza kutumikia kifungo chake.

Azania Post

Keywords:
Hispania
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.