Soko la hisa la Marekani laporomoka kiasi cha kutisha, mara baada ya tangazo hili

Sera za Rais Trump huenda zikaathiri uchumi wa nchi yake, hivyo kuwatisha wawekezaji

Soko la hisa la Marekani laporomoka kiasi cha kutisha, mara baada ya tangazo hili

Sera za Rais Trump huenda zikaathiri uchumi wa nchi yake, hivyo kuwatisha wawekezaji

28 June 2018 Thursday 10:58
Soko la hisa la Marekani laporomoka kiasi cha kutisha, mara baada ya tangazo hili

Na Mwandishi wetu

KUANZISHWA kwa ushuru wa forodha kwa bidhaa za Marekani katika bara la Ulaya tayari kumeanza kuyastua baadhi ya makampuni ya kigeni na kuamua kuondoa nchini humo.

Tayari kampuni ya Harley Davidson ya pikipiki ya Marekani imetangaza kuhamishia baadhi ya shughuli zake nje ya Marekani, ili kuepuka ushuru wa forodha utakaotozwa na Umoja wa Ulaya dhidi ya bidhaa za Marekani.

Baada ya kampuni hiyo kutangaza kuhamishia baadhi ya shughuli zake nje ya Marekani, soko la hisa nchini Marekani limeshuka kwa kiasi kikubwa, na thamani za kampuni tano kubwa za teknolojia za Marekani Facebook, Amazon, Apple, Netflix na Alphabet zimepungua kwa dola za kimarekani bilioni 80.

Hali hii imemkasirisha sana Rais Donald Trump wa Marekani, ambaye ameandika mara kadhaa kwenye Twitter akilaani kampuni ya Harley Davidson kwa kusalimu amri, na itaadhibiwa kwa kutozwa ushuru mkubwa na serikali ya Marekani hadi ifilisike.

Rais Trump anaona kuwa kampuni ya Harley Davidson iliyomsaidia kuwa rais wa Marekani ni mwakilishi hodari wa kampuni za Marekani, na madhumuni ya serikali ya Marekani kuongeza ushuru wa forodha kwa bidhaa za nchi za nje ni kuzilinda kampuni za Marekani kama Harley Davidson, na kuzihamasisha kurudisha viwanda na mitaji nchini Marekani.

Lakini sasa kitendo cha kampuni hiyo kinaenda kinyume na matarajio yake.

Lakini sababu halisi ya kampuni ya Harley Davidson kuhamishia baadhi ya shughuli zake nje ni vitendo vya kujilinda kibiashara vya serikali ya Marekani.

Umoja wa Ulaya ulitangaza kuongeza ushuru wa forodha wa pikipiki zinazotengenezwa na kampuni hiyo kuwa asilimia 31 kutoka 6, ili kulipiza kisasi vitendo vya kujilinda kibiashara vya Marekani. Baadaye bei ya pikipiki hiyo itaongezeka kwa dola za kimarekani 2,200 katika soko la Ulaya, na hali hii imelazimisha kampuni hiyo kuhamisha baadhi ya uzalishaji wake kutoka Marekani.

Ikiwa kampuni ya kwanza ya Marekani inayohamisha baadhi ya shughuli zake kutoka nchini humo, uamuzi wa kampuni ya Harley Davidson ni alama ya kushindwa kwa sera ya biashara ya serikali ya Trump.

Hivi leo kampuni za nishati, kilimo na uzalisajiezaji za Marekani zinakabiliwa na changamoto kubwa, kutokana na Umoja wa Ulaya, China, India, Uturuki, Mexico na nchi nyingine nyingi kutangaza hatua za kulipiza kisasi vitendo vya kujilinda kibiashara vya Marekani.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.