Taliban wakubali kusimamisha vita kupisha sikukuu ya Idd el Fitri

Ghani alitoa tangazo hilo kupitia televisheni ya taifa

Taliban wakubali kusimamisha vita kupisha sikukuu ya Idd el Fitri

Ghani alitoa tangazo hilo kupitia televisheni ya taifa

08 June 2018 Friday 10:54
Taliban wakubali kusimamisha vita kupisha sikukuu ya Idd el Fitri

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI ya Afghanistan imetangaza kusimamisha vita na waasi kupisha sikukuu ya Id el Fitri mwishoni mwa wiki ijayo.

Akizungumza Rais Ashraf Ghani wa nchi hiyo amesema usimamishaji mapigano na waasi wa Taliban utaanzia Jumanne ijayo hadi Juni 20, hatua inayoambatana na kukaribia kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Hata hivyo amesema mapigano dhidi ya makundi mengine kama lile la Dola la Kiislamu yataendelea.

Ghani alitoa tangazo hilo kupitia televisheni ya taifa.

Rais huyo alisema tangazo lake linaashiria nguvu za serikali ya Afghanistan na moyo wa umma katika kutafuta suluhisho la amani la mgogoro wa nchi hiyo.

Mkuu wa majeshi ya Afghanistan Jenerali Mohammad shariff Yaftali aliwaambia waandishi habari kwamba majeshi yake yatakuwa katika hali ya tahadhari, wakati wote wa usimamishaji mapigano.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.