Trump afanikiwa kuyazuia mataifa ya Kiislamu kuzuru Marekani

Ni baada ya mahakama kuidhinisha uamuzi wake

Trump afanikiwa kuyazuia mataifa ya Kiislamu kuzuru Marekani

Ni baada ya mahakama kuidhinisha uamuzi wake

28 June 2018 Thursday 10:54
Trump afanikiwa kuyazuia mataifa ya Kiislamu kuzuru Marekani

Na Mwandishi Wetu

MATAIFA yaliyo na idadi kubwa ya waislamu sasa huenda wakashindwa kutembelea Marekani mara baada ya mahakama ya juu nchini humo kuidhinisha marufuku ya Rais Donald Trump.

Imeripotiwa kuwa Mahakama hiyo imeidhinisha marufuku ya kusafiri, iliyotolewa na Rais Trump ikiyalenga mataifa yaliyo na idadi kubwa ya Waislamu.

Marufuku ya kusafiri, inayalenga mataifa yaliyo na idadi kubwa ya Waislamu. Mahakama hiyo ilitoa uamuzi wake siku ya Jumanne na kusema kwamba marufuku ya Trump, haivunji sheria za uhamiaji za Marekani.

Jaji mkuu John Roberts, aliandika katika maoni yake kwa mahakama kwamba rais, aliweka utetezi wa kutosha kuhusu usalama wa taifa kwa kuwazuia watu wengi wanaoingia Marekani, kutoka Somalia, Iran, Yemen, Syria, Libya, Chad, Korea Kaskazini na Venezuela.

Hata hivyo aliongeza kwamba mahakama haina mtizamo wowote juu ya uwazi wa sera. Uamuzi huo unadhihirisha kile kinachoonekana kuwa ushindi mkubwa wa kwanza wa sera za Trump tangu aingie madarakani Januari 2017.

Katika taarifa yake, Trump amesema uamuzi huo ni uthibitisho na ushindi mkubwa kwa watu wa Marekani.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.