Trump aitupilia mbali hatua ya kinyama aliyodhamiria kuichukua

Ni baada ya shinikizo kali kutoka kila upande

Trump aitupilia mbali hatua ya kinyama aliyodhamiria kuichukua

Ni baada ya shinikizo kali kutoka kila upande

21 June 2018 Thursday 17:28
Trump aitupilia mbali hatua ya kinyama aliyodhamiria kuichukua

Na Mwandishi Wetu

SHINIKIZO alilokuwa akipewa Rais Donald Trump wa Marekani kuhusu familia za wahamiaji nchini Mexico limezaa matunda.

Imeripotiwa kuwa Trump ameachana na sera yake ya kuzitenganisha familia za wahamiaji katika mpaka kati ya Marekani na Mexico kufuatia shinikizo kuhusu hatua hiyo iliyotajwa kuwa ya kinyama.

Trump ametia saini agizo linaloziruhusu familia za wahamiaji zizuiwe pamoja zinapokamatwa zikiingia Marekani kinyume na sheria hadi kesi zao zitakapoamuliwa.

Kiongozi huyo wa Marekani amesema lengo ni kuhakikisha familia hazitenganishwi lakini wakati huo huo, wanahakikisha mipaka inalindwa kwa mfumo madhubuti kuzuia mmiminiko wa wahamiaji nchini Marekani na kuwa alisikiza ushauri kutoka kwa mke wake Melania na binti yake Ivanka kufikia uamuzi huo wa kulegeza kamba.

Trump amesema amesikiliza kwa makini ushauri wa binti yake Ivanka ambaye pia ni mshauri wake kuhusu sera hiyo na kuongeza kuwa imezua hisia kutoka kwa kila aliye na imani na huruma akiwemo yeye.

Afisa mmoja wa Ikulu ya White House mjini Washington, amesema mke wa kiongozi huyo wa Marekani Melania, katika mazungumzo ya faragha na mume wake alimuomba achukue hatua kukomesha mzozo huo wa kibinadamu.

Mapema wiki hii, Melania pamoja na wake wa marais wa zamani wa Marekani walitoa wito wa kusitishwa kwa sheria hiyo ya kuwatenganisha wazazi wahamiaji na watoto wao wakisema Marekani inapaswa kuongozwa kwa kuzingatia sheria lakini pia kwa kuwa na imani.

Licha ya kuwa agizo hilo linafikisha kikomo sera ya kuzitenganisha familia iliyolaaniwa vikali na viongozi mbali mbalii akiwemo Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis na mashirika ya kutetea haki za binadamu, inamaanisha kuwa watoto watasalia vizuizini kwa muda usiojulikana.

Utawala wa Trump unakabiliwa na changamoto za kisheria kwa sababu uamuzi wa mahakama unawianisha kuwa maafisa wa uhamiaji wanaweza tu kuwazuia watoto kwa muda usiozidi siku ishirini na hilo huenda likachochea upya upinzani dhidi ya sera kali za Trump kuhusu uhamiaji, sera ambazo aliahidi kuzitekeleza wakati wa kampeini za uchaguzi wa rais mwaka.

Video zilizovujishwa wiki hii zilionesha watoto wakilia wakiwa vizuizini na kupelekea utawala wa Trump kulaaniwa vikali na Wamarekani na jumuiya ya kimataifa. Inakadiriwa zaidi ya watoto 2,000 walitenganishwa na wazazi wao katika kipindi cha wiki sita zilizopita kati ya tarehe 5 Mei na tarehe 9 mwezi huu.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.