Trump, Kim sasa kuzungumzia hotelini masuala nyeti ya nchi zao

Mkutano baina ya viongozi hao unatarajiwa kufanyika Juni 12 mwaka huu

Trump, Kim sasa kuzungumzia hotelini masuala nyeti ya nchi zao

Mkutano baina ya viongozi hao unatarajiwa kufanyika Juni 12 mwaka huu

06 June 2018 Wednesday 13:05
Trump, Kim sasa kuzungumzia hotelini masuala nyeti ya nchi zao

Na Mwandishi Wetu

MKUTANO unaosubiriwa kwa hamu na watu wengi duniani kati ya viongozi wa Marekani na Korea Kaskazini sasa utafanyika hotelini huko Singapore wiki ijayo.

Tayari Ikulu ya Marekani imetangaza kuwa Rais Donald Trump wa Marekani na Kiongozi mkuu wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, watakutana kwenye hoteli ya Capella iliyoko kwenye kisiwa cha Sentosa nchini Singapore.

Kabla ya hapo Rais Trump alisema mkutano kati yake na Bw. Kim Jong Un utakuwa ni mwanzo wa kitu kikubwa.

Wakati mkutano kati ya viongozi hao ukisubiriwa, Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo jana alikutana na mwenzake wa Singapore Bi. Vivian Balakrishan na kujadili mambo ya biashara, ushirikiano kati ya Marekani na nchi za ASEAN, na kuhusu mkutano unaotarajiwa kufanyika, kati ya rais Trump na Bw. Kim.

Bw. Pompeo ameishukuru Singapore kwa kukubali kuwa mwenyeji wa mkutano kati ya viongozi hao wawili.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.