Trump kukabidhiwa barua kutoka kiongozi wa Korea Kaskazini

Bado haijawekwa wazi kama mkutano baina ya Rais Trump na Kim Jong Un utafanyika Juni 12 kama ilivyopangwa awali

Trump kukabidhiwa barua kutoka kiongozi wa Korea Kaskazini

Bado haijawekwa wazi kama mkutano baina ya Rais Trump na Kim Jong Un utafanyika Juni 12 kama ilivyopangwa awali

01 June 2018 Friday 10:08
Trump kukabidhiwa barua kutoka kiongozi wa Korea Kaskazini

Na Mwandishi Wetu

RAIS wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kukabidhiwa barua yenye ujumbe maalum kutoka kwa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un huko jijini Washington leo.

Taarifa zinasema kuwa Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw Mike Pompeo amesema ofisa mwandamizi wa Korea Kaskazini anapanga kwenda Marekani na kuwasilisha barua ya kiongozi wa Korea Kaskazini kwa Rais Trump.

Bw. Pompeo amesema hayo katika mkutano na wanahabari mjini New York baada ya kumaliza mazungumzo ya siku mbili na ujumbe wa Korea Kaskazini unaoongozwa na naibu mwenyekiti wa kamati kuu ya Chama cha Wafanyakazi cha Korea Kaskazini Bw. Kim Yong Chol.

Bw. Pompeo amesema maendeleo yamepatikana kwenye mazungumzo na Korea Kaskazini yaliyofanyika mjini New York na sehemu nyingine.

Lakini amesema bado hajui kama mkutano wa marais wa nchi hizo mbili utafanyika nchini Singapore tarehe 12 mwezi Juni kama ilivyopangwa.

Shirika la Habari la Korea Kaskazini limeripoti kuwa kiongozi Kim amesema dhamira yake ya kuondoa silaha za nyuklia haibadiliki.

Aidha, wizara ya mambo ya muungano ya Korea Kusini imesema maofisa wake wa ngazi ya juu na Korea Kaskazini watafanya mazungumzo katika kijiji cha Panmunjom.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.