banner68
banner58

‘Tutaondoka Syria iwapo tu, Iraq na Syria watatutaka tufanye hivyo’ - Iran

Iran yatishia kuondoa majeshi ya Marekani kutoka Syria kwa nguvu

‘Tutaondoka Syria iwapo tu, Iraq na Syria watatutaka tufanye hivyo’ - Iran

Iran yatishia kuondoa majeshi ya Marekani kutoka Syria kwa nguvu

13 July 2018 Friday 15:12
‘Tutaondoka Syria iwapo tu, Iraq na Syria watatutaka tufanye hivyo’ - Iran

Mshauri mkuu wa Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei Ijumaa alisema Tehran ingeondoa majeshi yake kutoka Syria iwapo tu itatakiwa kufanya hivyo na dikteta Bashar Assad au serikali ya Iraq.

“Uwepo wa Iran na Urusi nchini Syria utaendelea kulinda nchi dhidi ya makundi ya kigaidi na uchokozi wa Marekani ... Tutaondoka mara moja ikiwa serikali za Iraq na Syria zinataka, si kwa sababu ya shinikizo la Israeli na Marekani, "alisema Ali Akbar Velayati, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.

Velayati alikuwa huko Moscow baada ya mazungumzo na Rais wa Urusi Vladimir Putin mapema wiki hii, ambayo yalikuja masaa kadhaa baada ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kukutana na kiongozi wa Urusi kushawishi kwa kuondolewa kwa askari wa Iran kutoka taifa hilo lililoharibiwa na vita ambalo lina mpaka na Israeli.

"Uwepo wetu Syria hauhusiani na Israeli," alisema Velayati Ijumaa, kulingana na shirika la habari la Urusi TASS.

"Sisi, bila shaka, tunawashirikisha Warusi na Wasyria juu ya mahali majeshi yetu yalipo. Ushirika huu sio lazima uendane na matakwa ya Israel."

Msaidizi wa ngazi za juu wa Iran pia alihatishia kutumia nguvu za kijeshi kuondosha askari wa Marekani kutoka Syria.

"Tutawashinda Wamarekani kwa nguvu," alisema.

"Tutawasaidia Syria kupambana na unyanyasaji wa Marekani. Ikiwa Marekani haitaki kuondoka kanda yetu, tutailazimisha kufanya hivyo. "

Marekani na Israeli zina wasiwasi juu ya uwepo kijeshi wa Iran huko Syria, ambapo imetoa msaada muhimu kwa majeshi ya Assad.

Israeli imesema mara kwa mara haitaruhusu Iran, au washirika wake wa Kishia, kuwepo ndani ya Syria baada ya vita.

Hali ya wasiwasi imekuwa ikizidi kuongezeka mpakani katika miezi ya hivi karibuni, huku Israel ikifanya mashambulizi dhidi ya majeshi ya Iran ndani ya Syria katika kujibu mapigo dhidi ya mashambulizi ya maroketi na ndege zisizo na rubani anbazo zimekuwa zikiingia ndani ya anga la Israel.

Sasa Tehran inaamini kuwa ina wapiganaji 80,000 nchini Syria - wanamgambo wa Kishia na vikosi vya wanamgambo vitiifu kwa Iran.

Urusi hata hivyo imesema kuwa sio rahisi kutegemea kuondoka kabisa kwa Iran kutoka nchini Syria, lakini kumekuwa na dalili za maelewano baina ya Moscow na Jerusalem juu ya suala hilo.

Siku ya Alhamisi, maafisa wa ngazi za juu wa Israeli walisema Urusi inafanya kazi ili kuzuia Iran kuweka mizizi yake kijeshi kwenye mpaka wake wa kaskazini na Syria.

Suala hilo linatarajiwa kuwa kiini cha mazungumzo baina ya Rais Donald Trump wa Marekani na mwenzake wa Vladimir Putin wa Urusi huko nchini Finland.

Siku ya Jumatano, wakati wa mkutano wao wa Moscow, Netanyahu alimwambia Putin kuwa Israeli haina mpango wa kumwondoa Assad madarakani, lakini aliwahimiza Urusi kufanya kazi ya kuondoa vikosi vya Iran kutoka nchini Syria, afisa wa Israeli alisema baada ya mkutano huo.

"Hatutachukua hatua dhidi ya utawala wa Assad, na uwaondoe Wairan," shirika la habari la Reuters lilimnukuu Netanyahu akimwambia Putin, akitoa mfano wa afisa.

Moscow ilishirikiana na Tehran kuimarisha utawala wa serikali ya Assad, lakini maslahi yao mara nyingi hayaendani. Urusi pia imekuwa na uhusiano wa karibu na Israeli na imeonyesha kuwa tayari kuzingatia maslahi ya kiusalama ya taifa hilo la Kiyahudi.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.