Uhamiaji wavigawa vyama vya siasa

Vyama vya CDU na CSU vyashindwa kuelewana

Uhamiaji wavigawa vyama vya siasa

Vyama vya CDU na CSU vyashindwa kuelewana

15 June 2018 Friday 15:15
Uhamiaji wavigawa vyama vya siasa

Na Mwandishi wetu

SERA ya uhamiaji imevigawa vyama vikubwa vya kihafidhina vya Ujerumani vya Christian Democratic Union - CDU na Christian Social Union – CSU.

Mgawanyiko huo unahusu kile kinachofahamika kuwa ni mpango mkubwa wa uhamiaji unaotayarishwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Horst Seehofer ambao unajumuisha kuwarudisha walikotoka baadhi ya watu kwenye mpaka wa Ujerumani - kitu ambacho Kansela Angela Merkel anakipinga waziwazi.

Baada ya msururu wa mikutano, Merkel amesema kuwa anatarajia kupata suluhisho kuhusu suala la uhamiaji ambalo alielezea kuwa mojawapo ya changamoto kubwa kabisa zinazoikabili Ulaya, sio tu Ujerumani.

Kwingineko, uchunguzi wa maoni uliofanywa na televisheni ya ARD, unaonyesha kuwa Wajerumani wengi wamesema kuwa itakuwa vibaya kama Merkel atasusia kwenda kuhudhria Kombe la Dunia nchini Urusi.

Asilimia 69 ya walioulizwa wanahisi kuwa kiongozi huyo wa nchi anapaswa kuwa Urusi kuiunga mkono timu yao wakati ikijaribu kulitetea taji lao la dunia.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.