UN yataja njia pekee kusuluhisha vita, yapongeza muda wa kusitisha mapigano

UN yataja njia pekee kusuluhisha vita, yapongeza muda wa kusitisha mapigano

17 June 2018 Sunday 15:08
UN yataja njia pekee kusuluhisha vita, yapongeza muda wa kusitisha mapigano

Na Mwandishi Wetu

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kuwa anakaribisha tangazo la serikali ya Afghanistan la kuongeza muda wa kusitisha mapigano na kundi la Taliban huku akihimiza wito wa amani kutoka kwa raia nchi hiyo kufuata nyayo za kusitisha mapigano pia.

Kupitia taarifa iliyotolewa leo na msemaji wake, Bw. Gutereres amesema, anaamini kuwa suluhisho pekee la vita nchini Afghanistan ni kupitia mchakato jumuishi wa kisiasa.

Ameongeza kuwa Umoja wa Mataifa upo tayari kufanya kazi na watu wa Afghanistan, Serikali ya Afghanistan na wadau wote ili kufikia amani ya kudumu nchini humo.

Aidha Bw, Guterres amehimiza pande zote kinzani kutoruhusu wale wanaojaribu kuchochea na kuvuruga mchakato wa amani unaoendelea, huku akilaani mashambulizi ya kigaidi yaliyofanyika hii leo katika mji wa Jalalabad-Torkham uliopo Mashariki mwa jimbo la Nangahar ambayo yaliwalega raia waliokuwa kwenye sherehe ya Eid na kukatili maisha ya watu 17 na wengine zaidi ya 10 kujeruhiwa.

Bwana Guterres ametuma salamu za rambirambi kwa familia za wafiwa na pia serikali ya Afghanistan na amewatakia ahuweni ya haraka majeruhi wa shambulio hilo.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.