Vita madawa ya kulevya yaleta vilio kila kona ndani ya wiki mbili tu

Vita madawa ya kulevya yaleta vilio kila kona ndani ya wiki mbili tu

29 May 2018 Tuesday 17:12
Vita madawa ya kulevya yaleta vilio kila kona ndani ya wiki mbili tu

Na Mwandishi Wetu

WASIWASI kuhusu haki za binadamu unazidi kuongezeka huko Bangladheshi mara baaada ya mamia ya watu kuuawa na wengine kukamatwa katika kipindi cha siku kumi na nne zilizopita.

Waliouwawa inasemekana walishukiwa kwa kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya ambayo haitakiwi kabisa nchini humo

Polisi inasema kwamba washukiwa kumi zaidi wanaodaiwa kuhusika na usafirishaji haramu wa dawa za kulevya walipigwa risasi mapema asubuhi ya jumanne baadhi wakiuwawa baada ya kupigwa risasi na polisi na wengine wakiuwawa katika kile kilichotajwa kuwa vita kati ya wafanyabiashara wa mtandao wa madawa ya kulevya.

Washukiwa jumla ya 102 wa kusafirisha madawa ya kulevya wameuwawa tangu Bangladesh ilipoanzisha mapambano makubwa dhjidi ya madawa ya kulevya katikati ya mwezi Mei yanayolenga kuisambaratisha kabisa biashara hiyo inayoongezeka nchini humo.

Waziri wa mambo ya ndani Asadduzzaman Khan ameliambia shirika la habari la AFP kwamba wanasimama kidete kuona vita hii inaendelea hadi pale watakapofanikiwa kuidhibiti kabisa.

Washukiwa kiasi 12,000 wamekamatwa na kushtakiwa katika mahakama maalum tangu yaliypoanzishwa mapambano ya kuwaandamana wanaohusika kuuza na kusafirisha madawa ya kulevya mnamo Mei 15 huku wengi wa watuhumiwa wakikutikana na hatia na kuhukumiwa vifungo kati ya siku saba hadi miezi sita jela.

Kwa mujibu wa waziri Khan waliouwawa katika vita hivyo hapana shaka walikuwa ni wafanyabiashara kabisa wa madawa ya kulevya licha ya kutolewa madai na makundi ya kutetea haki za binadamu kwamba watu wasiokuwa na hatia ndio waliouwawa.

Hata hivyo waziri huyo wa mambo ya ndani anasisitiza kwamba waliouliwa ni watu waliokuwa na bastola na walidiriki kufyatua risasi mara tu walipowaona polisi,na huo ni ushahidi tosha ulioonesha kwamba walikuwa sio watu wazuri .

Tume ya kutetea haki za binadamu nchini humo hata hivyo wiki hii imezungumzia wasiwasi wake mkubwa kuhusiana na kuongezeka idadi ya wanaouwawa na kutoa tahadhari kuhusu mauaji yanayofanywa kiholela bila kuzingatia sheria.

Kikosi maalum cha mapambano dhidi ya madawa ya kulenya kimesema watu 24 waliouwawa na polisi wa kikosi hicho walikuwa ni vinara katika mtandao wa biashara ya mihadarati ingawa pia kikosi hicho hakijatowa ushahidi wa hilo.

Miongoni mwa waliouwawa inatajwa yupo pia diwani kutoka jimbo la Teknaf ambaye wafuasi wake wanasema hakuwa na maingiliano yoyote na madawa ya kulevya.

Kwa upande mwingine waliouwawa leo Jumanne walikuwemo pia washukiwa wawili wanaodaiwa kuwa vinara wakuu wa mtandao wa biashara hiyo ambao walikutwa na polisi tayari wameshauawa.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.